Millard Ayo's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
Kikosi cha Yanga SC kimewasili leo jijini Dar es Salaam kikitokea Khartoum Sudan ambapo ilikwenda kucheza mchezo wa marudiano wa round ya kwanza dhidi ya Al Hilal ya Sudan, Yanga wameondolewa kwa kufungwa goli 1-0 hivyo wameaga michuano hiyo kwa aggregate ya 2-1, Yanga wanarejea Dar es Salaam wakisubiria kucheza play off ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya November 2 & 9 2022.
Simba SC imerejea Leo Dar es Salaam wakitokea Angola walipokwenda kucheza mchezo wao wa kwanza wa round ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya De Agosto ya Angola, Simba SC imefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1 ugenini.
Yanga SC leo wamecheza mchezo wao wa round ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kutoka sare 1-1.
Yanga SC leo imeibuka na ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini katika mchezo wa marudiano wa Club Bingwa Afrika, Yanga wanaitoa Zalan kwa aggregate ya magoli 9-0, huku staa wao Fiston Mayele akipiga hat-trick mbili mfululizo.