|
Soka360's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“For comprehensive coverage of Tanzanian soccer 🇹🇿 contact soka360tz@outlook.com” Report User |
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kimefanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Niger kesho saa 10:00 jioni uwanja wa Benjamin mkapa.
#LigiKuu | Klabu ya Azam imethibitisha kuwa hakutakuwa na kiingilio kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Polisi Tanzania Azam Complex kama sehemu ya shukrani kwa mashabiki wao kwa kuwa pamoja kwa msimu mzima Aidha getini kila shabiki atapatiwa kinywaji cha Azam Mango Crush
#LigiKuu | Kuelekea mchezo dhidi ya Azam Saido Ntibanzonkiza na Moses Phiri ndio vinara wa mabao kwa upande wa Simba. Wana mabao 10 kila mmoja. Je kesho wataongeza idadi ya mabao kwenye akaunti zao?
#LigiKuu | Simba wamefanikiwa kushinda kwenye michezo yao mitano iliyopita. Ambapo wamekusanya alama 15 kwenye mechi 5 za mwisho. Kesho anakutana dhidi ya Azam,Je ataendeleza kutoa dozi?
#LigiKuu | SIMBA vs AZAM. Simba amepoteza mchezo mmoja mpaka sasa na amepoteza dhidi ya Azam ambao waliwafunga bao 1-0 Wanakutana tena kwa Mkapa ambapi Simba wapo nafasi ya 2 na alama 53,Michezo 22. Huku Azam wakiwa nafasi ya 4 na alama zao 43,michezo 22. Nani atatoboa kesho?
#LigiKuu | Hapa ni Highland Estate-Mbarali,Mbeya😊, Uwanja wa nyumbani wa Klabu ya Ihefu ambayo leo inacheza mchezo dhidi ya Mbeya City muda mfupi ujao. Meneja wa Uwanja huu bwana Malule Omary ndiye alitwaa tuzo ya meneja bora wa Uwanja kwa mwezi januari 2023. Amestahili💪