Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison ameanza kuitia hofu Jwaneng Galaxy, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya Kwanza utakaochezwa mwishoni mwa juma hili mjini Gaborone, Botswana. Simba SC itaanzia ugenini Oktoba 17, kisha itarejea nyumbani jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo wa Mkondo wa pili uliopangwa kucheza Oktoba 22, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam. Jina la Morrison limetajwa na Kocha Mkuu wa Jwaneng Galaxy Morena Ramoreboli, kama mmoja wa wachezaji hatari wa Simba SC na anatakiwa kuchungwa sana kwenye michezo yote miwili. -- Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali. JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA DAR24 MEDIA: +255 679 979 786 ⚫️ Email: dar24news@gmail.com ⚫️ Website: www.dar24.com ⚫️ Instagram: @Dar24Tz ⚫️ Facebook: @dar24news ⚫️ Twitter: @Dar24News #bernardmorrison#simbasc #hajimanara
TIMU ya taifa ya Tanzania leo Oktoba 10 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia. Nahodha Mbwana Samata alishuhudia kijana wake Simon Msuva akipachika bao la ushindi mapema dakika ya 6 na lilidumu mpaka dakika ya 90. Katika mchezo wa leo Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ilicheza kwa utulivu mkubwa na kusaka ushindi wa haraka kipindi cha kwanza na baada ya kupata ushindi kazi ya ulinzi na kushambulia kwa kushtukiza iliendelea. Beki wa Stars, Kennedy Juma ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakitumia nguvu nyingi jambo lililopelekea akaonyeshwa kadi ya njano. Ushindi huo unaifanya Stars kufukisha pointi saba sawa na Benin katika kundi J ikiwa inaongoza kwa wakati huu na itafahamika baada ya mchezo wa Dr Congo wenye pointi 5 ambao watacheza na Madagascar ambayo haijakusanya pointi mpaka wakati huu.
Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://bit.ly/2Q3HICf Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCsports #KenyaSports #Football
Follow us on: Twitter(https://twitter.com/football_kenya) Instagram (https://www.instagram.com/football_kenya) Like our Facebook page (https://www.facebook.com/FootballKenyaFederation) #HarambeeStars|#IsupportStars|#HarambeStarlets