#inkmediatz #africanfootballleague
Kikosi cha Al-Ahly kimetua Tanzania kumenyana na Simba kwenye Mchezo wa AFL dhidi ya Simba ambae ndio mwenyeji wa Mchezo huo. Balozi wa Misri Nchini Tanzania Sharif Ismail amezungumza baada ya Kikosi cha Al-Ahly kutua Tanzania. Mapokezi yao na baadhi mipango yote ya Mechi Balozi amezungumza hapa
Baada ya Kimya kirefu hatimae Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC Hasheem Ibwe ameibuka tena na kuutangazia umma kuwa wanautaka Ubingwa Msimu. Ibwe amezungumza kinachoendelea kwenye Kikosi cha Azam FC Wakati huu ambao Ligi imesimama pamoja na Nyota wanatarajia kurejea hivi karibuni. Aidha ametoa shukrani kwa Timu iliyowauzia Feisal Salum kwani walichotaka akifanye ndio anakifanya kwa sasa kwenye Kikosi cha Azam FC. Pia ametoa maoni yake juu ya Michuano ya AFL ambao Simba wanakwenda kufungua Pazia dhidi ya Al-Ahly kutoka Misri, ambapo Ibwe amewatakia Simba lolote liwakute kwani adui yake hawezi kumuombea mema. Sanjari na hayo ametuma salam kwa Baraka Mpenja kuwa asitishie kuacha kutangaza kwani Mashabiki wa Soka bado wanataka burudani.
Hatimaye Pyramids FC ya Misri imetangaza kumsajili Mshambuliaji FISTON MAYELE kutoka Yanga SC. Nayo Klabu ya Yanga imemuaga rasmi Mayele na kumshukuru kwa huduma yake ya miaka miwili.