IBWE AWAOMBEA SIMBA LOLOTE LIWAKUTE/"SISI NI DHAHABU/YANGA WANAMUOTA FEISAL/MPENJA ASIENDE UMALILA by @Mpenja TV - Post Details

IBWE AWAOMBEA SIMBA LOLOTE LIWAKUTE/"SISI NI DHAHABU/YANGA WANAMUOTA FEISAL/MPENJA ASIENDE UMALILA

Baada ya Kimya kirefu hatimae Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC Hasheem Ibwe ameibuka tena na kuutangazia umma kuwa wanautaka Ubingwa Msimu. Ibwe amezungumza kinachoendelea kwenye Kikosi cha Azam FC Wakati huu ambao Ligi imesimama pamoja na Nyota wanatarajia kurejea hivi karibuni. Aidha ametoa shukrani kwa Timu iliyowauzia Feisal Salum kwani walichotaka akifanye ndio anakifanya kwa sasa kwenye Kikosi cha Azam FC. Pia ametoa maoni yake juu ya Michuano ya AFL ambao Simba wanakwenda kufungua Pazia dhidi ya Al-Ahly kutoka Misri, ambapo Ibwe amewatakia Simba lolote liwakute kwani adui yake hawezi kumuombea mema. Sanjari na hayo ametuma salam kwa Baraka Mpenja kuwa asitishie kuacha kutangaza kwani Mashabiki wa Soka bado wanataka burudani.

Similar Posts!