#SimbaSC #UdSongo #SoccerData Wikiendi hii Simba ilicheza mechi ya Kimataifa dhidi ya UD Do Songo ya Nchini Msumbiji, ikiwa ni mechi ya marudiano katika mashindano ya ligi ya mabaingwa Afrika hatua ya mchujo yaani preliminary stage. Katika matokeo ya awali Simba ilitoka sare tasa, hivyo katika mchezo wa marudiano Simba ilihitaji ushindi wowote ule. Simba imetoka sare pacha ya goli moja kwa moja, na kuilazimisha Simba kutupwa nje ya mashindano. Ud Songo wamepita hatua hii na sasa watakutana na FC Platnum kwa faida ya goli la ugenini. Channeli inakuletea Uchambuzi wa kiufundi wa mechi hii, hapa utapata kujua mbinu za walimu wa timu zote mbili, wapi kulikuwa na udhaifu, vikosi vya timu zote mbili, na ni kwanini Simba ilipata matokeo iliyoyapata, walikwama wapi kimbinu na kimkakati. Ungana na chaneli hii sasa kwa KU SUBSCRIBE NA KISHA bofya alama ya Kengele, kufanya hivyo kutakufanya usikose video zingine za kiuchambuzi zenye lengo la kuweka mambo sawa kiufundi.
IKICHEZA kwa kujiamini na mbinu za hali ya juu, juzi Jumamosi Simba ililazimisha suluhu ugenini dhidi ya wenyeji, UD Songo ya Msumbiji. Katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Beira, Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisisitiza kwamba; “Tunakwenda kumaliza kazi Dar.” Simba iliandika rekodi ndani ya msimu mpya baada ya kutoruhusu bao lolote ikianzia mashindano hayo makubwa ugenini. Msimu uliopita kwenye hatua ya awali Simba ilianzia nyumbani dhidi ya Mbabane ikashinda 4-1, ugenini ikashinda mabao 4-0. Baada ya hapo katika mechi zote ilizocheza ugenini ikaruhusu mabao mengi. Katika mchezo wa jana Simba ilionekana kucheza kwa kujiamini huku safu ya ulinzi ikifanya kazi ya ziada. Ndani ya dakika 45 za kwanza Simba ilipiga mashuti matatu ambayo hayakuwa na madhara lakini mengine mawili nusura yawaamshe mashabiki kwani kipa alipangua yakawa kona. Wekundu hao walipata kona nne za haraka huku wakionekana kutawala zaidi eneo la katikati na kuwalazimisha wenyeji kupiga pasi ndefu ambazo hata hivyo walionyesha udhaifu mkubwa kwenye umaliziaji kwani walikuwa wakipaisha au kupiga pasi fyongo ambazo zilikuwa mboga kwa Benno Kakolanya. UD Songo walicheza mpira wa kuvizia kipindi cha pili lakini wakadhibitiwa na Nyoni na Wawa ambao walionekana kujiamini. Shiboub ambaye ni raia wa Sudan katika mechi jana alitawala kiungo na kuziba mianya mingi ya wenyeji kuwafikia mabeki wa Simba. Mkude muda mwingi alikuwa akiinasa mipira, kuidhibiti na kumpa Chama ambaye kazi yake ilikuwa kusambaza tu. Kwa mujibu wa kocha na viongozi wa Simba, uwanja uliochezwa mechi hiyo wa Campo Do Ferroviario Da Beira ulikuwa chakavu sana na haukuruhusu kucheza kiwango chao ingawa suluhu bado inawabeba. Aussems alisisitiza kwamba wana nafasi kubwa ya kushinda Dar es Salaam kwenye mechi ya marudiano na kusonga mbele na hawana wasiwasi. “Ulikuwa mchezo wa wazi, walikuwa wakijaribu kufunga na kwetu ilikuwa hivyo, jambo muhimu hatujaruhusu goli. Mchezo wa marudiano utakaochezwa Dar ni muhimu, kwa ushangiliaji wa mashabiki wetu na uwanja mzuri nafikiri tutafanya vizuri,” alisema Kocha Aussems.
TAIFA STARS KUUMANA TENA NA KENYA, TFF WAMETANGAZA..! Shirkisho la soka Tanzania TFF limesema mashindano ya Chani yanatarajiwa kuanza siku ya tarehe 28 ya mwezi huu ambapo Stars itaanza kibarua chake cha kwanza, dhidi ya Kenya kisha marudiano ilii kuhakikisha kufudhu mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika nchini CAMEROON #TAIFASTARS #TFF #CHANI Https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
BAADA ya kupoteza mchezowake wa jana kwa kufungwa mabao 2-1 na Simba, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nswanzurimo amesema kuwa kinachoiponza Simba kupokea vichapo ikiwa nje kwenye mashindano ya kimataifa ni kubebwa na waamuzi ambao wanashindwa kutafsri sheria 17.#Simba
Siri ya SIMBA kupigwa ( 4 -1 ) na TP MAZEMBE Yafichuka! Kocha wa simba Patrick Aussems amefichua sababu ya wao kupoteza mechi ya robo fainali ya pili na kutupwa nje ya mashindano ya vilabu bingwa Afrika na mabingwa mara tano wa kombe hilo timu ya TP Mazembe baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-1 ugenini nchini Congo DRC https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
#Simba #Tpmazembe Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Simba imepoteza mchezo wake wa robo fainali ya marudiano huku ikiondolewa kwenye mashindano hayo ya Afrika. Mchezo wake wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars