Content removal request!


SIMBA KUTOLEWA: SAbabu 5 za kiufundi hizi hapa-Aussems/ Kahata/ Shiboub.

#SimbaSC #UdSongo #SoccerData Wikiendi hii Simba ilicheza mechi ya Kimataifa dhidi ya UD Do Songo ya Nchini Msumbiji, ikiwa ni mechi ya marudiano katika mashindano ya ligi ya mabaingwa Afrika hatua ya mchujo yaani preliminary stage. Katika matokeo ya awali Simba ilitoka sare tasa, hivyo katika mchezo wa marudiano Simba ilihitaji ushindi wowote ule. Simba imetoka sare pacha ya goli moja kwa moja, na kuilazimisha Simba kutupwa nje ya mashindano. Ud Songo wamepita hatua hii na sasa watakutana na FC Platnum kwa faida ya goli la ugenini. Channeli inakuletea Uchambuzi wa kiufundi wa mechi hii, hapa utapata kujua mbinu za walimu wa timu zote mbili, wapi kulikuwa na udhaifu, vikosi vya timu zote mbili, na ni kwanini Simba ilipata matokeo iliyoyapata, walikwama wapi kimbinu na kimkakati. Ungana na chaneli hii sasa kwa KU SUBSCRIBE NA KISHA bofya alama ya Kengele, kufanya hivyo kutakufanya usikose video zingine za kiuchambuzi zenye lengo la kuweka mambo sawa kiufundi.