SUBSCRIBE HAPO JUU tembelea WEBSITE YETU https://bmtvtanzania.com/ INSTAGRAM https://www.instagram.com/bmtvtanzania FACEBOOK https://www.facebook.com/bmtvtanzania TWITTER https://twitter.com/bmtvtanzania1
Mabadiriko ya uwanja utakaotumika katika mechi kati ya simba na Mwadui, Yametajwa na manara wakati akizungumza na waandishi wa habari. hata hivyo timu hizo zinakutana zikiwa na kumbukumbu ya simba kufungwa Goli 1:0 na Mwadui, lakini Simba inaibuka na kusema lazima ilipe kisasi. fuatilia mechi hiyo kupitia channel hii na usisahau kuSUBSCRIBE. #SIMBAVSMWADUI #MANARA #UWANJAWATAIFA Baada ya kuvuna pointi sita muhimu katika michezo miwili ya Ligi Kuu Bara huko Kanda ya Ziwa, kikosi cha Simba jana kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA, huku kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya akiwemo kati yao. Simba inajianda na mechi ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii. Katika mchezo huo, Simba wataingia uwanjani wakiwa na hasira za kufungwa katika mchezo wa ligi uliopigwa Uwanja wa Kambarage huko Shinyanga ambao ulimalizika kwa Mwadui kushinda bao 1-0. Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja Mkuu wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema kuwa kikosi chao kitaingia kambini leo jioni huko Ndege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Rweyemamu alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na wachezaji wote wataingia kambini tayari kwa kuwawinda Mwadui kwa ajili ya kulipa kisasi cha kufungwa katika ligi. Aliongeza kuwa kiungo wao wa zamani Kichuya huenda akawa katika sehemu ya wachezaji watakaoingia kambini baada ya hivi karibuni kusaini mkataba wa kuichezea Simba. “Kesho (jana), timu yetu itaingia kambini rasmi huko Ndege Beach tulipoweka kambi ya kudumu katika msimu huu kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Mwadui. “Tunafahamu umuhimu mkubwa wa kombe hili, hivyo ni lazima timu yetu ipate matokeo mazuri ili tuendelee na mashindano hayo na mwisho wa siku tuweze kuchukua kombe hilo. “Maandalizi yanakwenda vizuri na timu yetu na wachezaji wote wataingia kambini kujiandaa na mchezo huo, pia Kichuya huenda akawa sehemu ya wachezaji watakaoingia kambini kama atakuwa amekamilisha baadhi ya vitu vyake kati yake na uongozi baada ya kusaini mkataba Simbva,” alisema Rweyemamu ambaye ni miongoni mwa wanachama wanaoaminika sana na uongozi wa juu wa Simba. SIMBA INATAKA KUWEKA REKODI
MASHABIKI wa Simba Walivyocheza Kigoma Wakirudi DAR Unaweza kusema mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kawatajirisha wauzaji wa jezi mkoani hapa kufuatia jezi yake kuuzwa kwa wingi. Licha ya uwepo wa jezi nyingi za Simba na Lipuli, lakini mashabiki wengi walikuwa wakiinunua jezi ya Kagere jambo ambalo wauzaji walilifurahia sana. Hali hiyo ilitokea muda mchache kabla ya jana Simba haijacheza na Lipuli kwenye Uwanja wa Samora uliopo hapa Iringa ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Championi ambalo lilipiga kambi katika eneo ambalo jezi hizo zinauzwa nje ya Uwanja wa Samora, lilishuhudia mwanzo mwisho uuzaji wa jezi hizo ukienda kwa kasi. Mmoja wa wauzaji wa jezi hizo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, alisema: “Jezi hapa zinauzwa kwa bei tofauti, hizi za Simba Sh 25,000 na za Lipuli Sh 15,000. Lakini huwezi amini jezi ya Kagere ndiyo inanunuliwa sana. Hapa kila mmoja ameuza si chini ya jezi 20 za Kagere.” https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
SPOTI HINTS: OKWI, JUUKO OUT! AFRICAN LYON VS SIMBA LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa michezo mbalimbali kupigwa katika viwanja Tofauti ikiwemo Mechi kati yaAfrican Lyon dhidi ya Simba katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha huku Kocha Mkuu Patrick Aussems akithibitisha kuwakosa wachezaji wake Emmanuel Okwi na Juuko Murshid. Lakini pia gumzo ambalo lilikuwa likiendelea katika mitandao ya kijamii ikimuhusu Beki Mkongwe Kelvin Yondani kutompa mkono Nahodha wake Ibrahim Ajibu leo wanayanga wameamua kuonyesha video ambayo inawaonyesha wako sawa huku wakikimbizana katika kambi yao waliyoweka jijini Mwanza wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbao FC. #OKWI #JUUKO https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
Baada ya Tanzania kupoteza mchezo wa kufuzu AFCON mwakani kwa kufungwa bao 1-0 na Lesotho, Kocha Mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike amesema anaumizwa na matokeo hayo huku akiwataka watanzania kutokata tamaa. Akijibu malalamiko ya baadhi ya wadau kuhusu aina ya kikosi alichokipanga, Amunike amesema alipanga wachezaji ambao walionesha uwezo mazoezini katika kambi ya siku iliyofanyika nchini Afrika Kusini, na hapangi kwa kuangalia majina ya timu wanazotoka.
Novemba 18 mwaka huu Tanzania inaweza kuandika historia mpya katika ulimwengu wa soka, kwani huenda ikafuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa barani Afrika mwakani nchini Cameroon, endapo itaifunga Lesotho. Mchezo huo utapigwa mjini Maseru nchini Lesotho na tayari kikosi cha Taifa Stars kimeshawasili nchini humo kikitokea nchini Afrika Kusini kilipokuwa kimeweka kambi yake. Katika kipindi hiki cha Viwanjani Novemba 16, 2018 tunajadili uwezekano wa timu hiyo ya Taifa ya Tanzania kushinda mchezo huo, huku tukitarajia Uganda iifunge Cape Verde na kurejea historia hiyo ya mwaka 1980. Studio tupo na wachambuzi Ezekiel Kamwaga na Gift Macha wakiongozwa na Alwaatan Ramadhan Ngoda.
Azam FC leo imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Express ya Uganda, mchezo ukipigwa jijini Kampala ambako Azam wameweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi. Matokeo ya mchezo huo ni sare ya bao 1-1 ambapo Azam ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Danny Lyanga dakika ya 15, huku Express wakisawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Matovu Roben.