Baada ya Tanzania kupoteza mchezo wa kufuzu AFCON mwakani kwa kufungwa bao 1-0 na Lesotho, Kocha Mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike amesema anaumizwa na matokeo hayo huku akiwataka watanzania kutokata tamaa. Akijibu malalamiko ya baadhi ya wadau kuhusu aina ya kikosi alichokipanga, Amunike amesema alipanga wachezaji ambao walionesha uwezo mazoezini katika kambi ya siku iliyofanyika nchini Afrika Kusini, na hapangi kwa kuangalia majina ya timu wanazotoka.