Content removal request!


MAGOLI: Express FC 1-1 Azam FC (Mechi ya kirafiki 12/08/2018)

Azam FC leo imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Express ya Uganda, mchezo ukipigwa jijini Kampala ambako Azam wameweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi. Matokeo ya mchezo huo ni sare ya bao 1-1 ambapo Azam ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Danny Lyanga dakika ya 15, huku Express wakisawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Matovu Roben.