Magoli | Tabora United 0-3 Yanga SC | NBC Premier League 02/04/2025
Magoli | Tabora United 0-3 Yanga SC | NBC Premier League 02/04/2025

Magoli kutoka kwa Israel Patrick Mwenda, Clement Mzize na Prince Dube yameipa Yanga ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC ukipigwa kwenye Dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Hiki ni kisasi kwa Yanga dhidi ya Tabora United, ikikumbkwa mchezo wa kwanza waliokutana msimu huu, Yanga ilipoteza nyumbani kw akichapo cha mabao 3-1 kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.



Tabora United 0-3 Simba SC | Highlights | NBC Premier League - 02/02/2025
Tabora United 0-3 Simba SC | Highlights | NBC Premier League - 02/02/2025

Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya NBC Premier League kati Tabora United dhidi ya Simba SC. Simba imeshinda kwa jumla ya magoli 3-0, Magoli yamefungwa na Leonel Ateba na Shomari Kapombe



Magoli | Tabora United 2-1 Azam FC | NBC Premier League 13/12/2024
Magoli | Tabora United 2-1 Azam FC | NBC Premier League 13/12/2024

Azam FC imekula mweleka ikipokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Tabora United mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara kwenye Dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Heritier Makambo amefunga goli la kwanza kwa tabora United na kusababisha goli la pili ambalo golikipa Mohamed Mustafa amejifunga...... Goli pekee la Azam FC limefungwa na beki Yoro Diaby.



Yanga SC 1-3 Tabora United | Highlights | NBC Premier League 07/11/2024
Yanga SC 1-3 Tabora United | Highlights | NBC Premier League 07/11/2024

Yanga SC imepoteza mchezo wa pili mfululizo kwenye ligi baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo Azam Complex, Chamazi. Offen Chikola amefunga magoli mawili dakika ya 19 na 45 ... huku Nelson Munganga akifunga la tatu dakika ya 78. Goli la kufutia machozi kwa Yanga limefungwa na Clement Mzize dakika ya 90. Yanga pia walipata penati dakika ya 45 ikipigwa na Stephane Aziz ki lakini ikadakwa na golikikpa Hussein Masalanga....



Magoli sita | JKT Tanzania 4-2 Tabora United | NBC Premier League 18/10/2024
Magoli sita | JKT Tanzania 4-2 Tabora United | NBC Premier League 18/10/2024

John Bocco amefunga magoli mawili dakika ya 21 na 26, akiiongoza JKT Tanzania kuichapa Tabora United mabao 4-2 ,katika mchezo wa #NBCPremierLeague uliopigwa kwenye Dimba la Meja Jenerali Isamuhyo. Dar es Salaam. Magoli mengine yametoka kwa Edward Songo dakika ya 58 na Said Ndemla dakika ya 63... huku magoli ya Tabora United yakifungwa na Offen Chikola dakika ya 42 na Yacouba Sogne dakika ya 90. Haya hapa magoli yote sita....



Simba SC 2-0 Tabora United | Highlights | NBC Premier League 06/05/2024
Simba SC 2-0 Tabora United | Highlights | NBC Premier League 06/05/2024

Simba SC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Magoli ya Simba yametoka kwa Sadio Kanoute dakika ya 19 na Edwin Balua dakika ya 77.




Next »


Popular Tags

#Cleveland Cavaliers  #David Silva  #Paul Pogba  #New York Knicks  #Best Champions League  #Zlatan Ibrahimovi  #Lionel Messi  #Luis Suarez  #Stephen Curry  #Chicago Bulls  

Popular Users

#Kaepernick7  #RobGronkowski  #JasonDufner  #PMOIndia  #iamsrk  #BillGates  #shakira  #NiallOfficial  #hunterpence  #jadande  #BrunoMars  #incarceratedbob  #RobbieSavage8  #ATLHawks  #tigerwoods