Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Simba imeitwanga Coastal Union kwa mabao 8-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Pamoja na ushindi wake mnono, washambuliaji wake wawili, Emmanuel Okwi na Meddy Kagere kila mmoja amefunga mabao matatu, yaani hat trick. Kwa mabao hayo, Kagere amefikisha mabao 20 msimu katika ligi kuu huku Okwi akifikisha 14 na kulingana na nahodha wa Simba, John Bocco aliyekuwa benchi katika mechi ya leo. Mabao mengine yalifungwa na Hassan Dilunga na Cleotus Chama raia wa Zambia na kuifanya Simba iandike ushindi huo mnono zaidi. Kwa ushindi wa leo, Simba imefikisha pointi 81 na kupaa kileleni ikiwaacha Yanga wenye pointi 80 waliokuwa wamekaa kileleni kwa muda mrefu zaidi. Yanga wamecheza 34 huku Simba wakiwa wamefikisha mechi 31 baada ya kucheza mechi yao ambayo wametoa kipigo kikali kwa Wagosi wa Kaya. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars
KOCHA MBEYA CITY Atoa POVU Baada ya Matokeo MBEYA CITY VS SIMBA 1 -2 KOHA Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo amesema kuwa hawajafungwa na Simba bali wamefungwa na waamuzi wa mchezo ambao wameshindwa kutimiza sheria 17. Mbeya City wamepoteza mchezo wa leo kwa kufungwa mabao 2-1 licha ya kuanza kutangulia kufunga kipindi cha kwanza kupitia kwa Iddy Nado ambaye alitumia makosa ya mabeki wa Simba waliokuwa wakikaba kwa macho. Nsanzurwimo amesema kuwa hajajua sababu ya faulo ya pili ambayo Simba wamepewa licha ya kuutazama mchezo kwa umakini hali iliyofanya wapoteza mchezo wao. "Hii ni kazi ya mtu, sasa kama inatokea mtu mwingine anaiharibu kwa makusudi hii sio sawa, ilikuwa ni lazima tushinde na tulipambana kweli matokeo yake Simba inashinda mabao 2-1 siamini kama nimefungwa na Simba bali nimefungwa na waamuzi. "Najua Simba ni timu kubwa ila haipaswi kupewa kipaumbele kila mara hata kama inakosea, ukitazama mabao yao na namna ambavyo wamefunga sina namna ya kukubali na kuwaomba waamuzi wawe makini wakati mwingine, vijana wangu wamechoka kwa kupambana kisha haki yao inapotea," amesema. Mabao ya Simba ya leo yote mawili yalifungwa kwa kutengenezwa na adhabu ambapo lile la kwanza lilifungwa na Jonas Mkude baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na la pili lilifungwa na Meddie Kagere baada ya Hassan Dilunga kuchezewa faulo. https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho