KOCHA MBEYA CITY Atoa POVU Baada ya Matokeo MBEYA CITY VS SIMBA 1 -2 KOHA Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo amesema kuwa hawajafungwa na Simba bali wamefungwa na waamuzi wa mchezo ambao wameshindwa kutimiza sheria 17. Mbeya City wamepoteza mchezo wa leo kwa kufungwa mabao 2-1 licha ya kuanza kutangulia kufunga kipindi cha kwanza kupitia kwa Iddy Nado ambaye alitumia makosa ya mabeki wa Simba waliokuwa wakikaba kwa macho. Nsanzurwimo amesema kuwa hajajua sababu ya faulo ya pili ambayo Simba wamepewa licha ya kuutazama mchezo kwa umakini hali iliyofanya wapoteza mchezo wao. "Hii ni kazi ya mtu, sasa kama inatokea mtu mwingine anaiharibu kwa makusudi hii sio sawa, ilikuwa ni lazima tushinde na tulipambana kweli matokeo yake Simba inashinda mabao 2-1 siamini kama nimefungwa na Simba bali nimefungwa na waamuzi. "Najua Simba ni timu kubwa ila haipaswi kupewa kipaumbele kila mara hata kama inakosea, ukitazama mabao yao na namna ambavyo wamefunga sina namna ya kukubali na kuwaomba waamuzi wawe makini wakati mwingine, vijana wangu wamechoka kwa kupambana kisha haki yao inapotea," amesema. Mabao ya Simba ya leo yote mawili yalifungwa kwa kutengenezwa na adhabu ambapo lile la kwanza lilifungwa na Jonas Mkude baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na la pili lilifungwa na Meddie Kagere baada ya Hassan Dilunga kuchezewa faulo. https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho