Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya leo kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam. Walioitafuna miwa ya Mtibwa kwenye mchezo huo uliokuwa mzuri na wa kuvutia, ni John Bocco dakika ya 33, Clatous Chama dakika ya 48 na Emmanuel Okwi dakika ya 56. Ushindi huo umefanya Simba ifikishe pointi 85 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwaacha Yanga kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 83 wakati Mtibwa Sugar wakisalia kwenye nafasi ya tano na pointi 49.
SUBSCRIBE HAPO JUU tembelea WEBSITE YETU https://bmtvtanzania.com/ INSTAGRAM https://www.instagram.com/bmtvtanzania FACEBOOK https://www.facebook.com/bmtvtanzania TWITTER https://twitter.com/bmtvtanzania1
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Kocha wa Azam FC, Meja Abdul #Mingange amesema, kikosi chao cha #AzamFC hakijafikia malengo waliyokusudia labda wachukue ubingwa wa FA utakaowapa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na akaweka wazi kuwa suluhu yao na Simba imewapata walichotaka. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Amesema, malengo ya Azam FC yalikuwa ni kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara au wamalize nafasi ya pili kwa sababu timu yao ni kubwa. "Katika msimu huu sisi hatujafanya vizuri kwa sababu tulitakiwa kuchukua ubingwa au nafasi ya pili lakini kama tutachukua ubingwa wa FA angalau tutakuwa tumefanya kitu,"alisema Mingange aliyechukua mikoba ya kuinoa Azam FC baada ya kutimuliwa Kocha Mholanzi Hans Pluijm. Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars "Wenzetu Simba walikuwa wanatafuta ubingwa lakini sisi hatuko huko hivyo hatukutaka kujichosha ndiyo maana tulicheza kwa kuzuia ili tusifungwe hivyo tumepata tulichokitaka,"alisema Mingange. Hata hivyo, Mingange amesema mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha Uwanja wa Uhuru ambao walichezea mechi kujaa maji uliwaathiri wao na wapinzani wao. Twitter: https://twitter.com/kidanistars Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei/John Bocco dk79, Haruna Niyonzima, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Clatous Chama. Azam FC; Razack Abalora, Nickolas Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Joseph Mahundi, Frank Domayo, Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Ramadhan Singano/Daniel Lyanga dk53.
#SIMBASC #AZAMFC Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Kikosi kitakachoanza: Aishi Manula, Nicholous Gyan,Mohamed Hussein, Yusufu Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei, Haruna Niyonzima, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi, Clatous Chama Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Deogratius Munish, Zana Coulibary, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, John Bocco, Rashid Juma Akiba: Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars
KIKOSI cha Maangamizi cha SIMBA VS KAGERA SUGAR Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa Simba kuendelea kuwa kibonde wa Kagera Sugar baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0. Bao pekee la mchezo huo limepatikana mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza kwa Mohammed Hussein kujifunga ikiwa ni baada ya kukosa mawasiliano mazuri baina yake na kipa Aishi Manula kufuatia mpira uliopigwa na mchezaji wa Kagera. Licha ya kutawala sehemu kubwa ya mchezo, Kagera Sugar walionekana kulinda kwa umakini zaidi lango haswa baada ya kupata bao la kuongoza na kuwafanya Simba kushindwa kucheka na nyavu zao. Kunako kipindi cha pili cha mchezo, Kocha wa Simba Patrick Aussems aliwafanyia mabadiliko wachezaji Hassan Dilunga aliyemtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Rashid Juma huku James Kotei naye akitolewa na Jonas Mkude akichukua nafasi yake. Mabadiliko hayaikuisaidia chochote Simba ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalisalia kuwa 1-0. Kuendelea kupoteza kwa Simba dhidi ya Kagera kunawafanya wazidi kusalia nafasi ya kwanza wakiwa na alama zao 81 kwenye nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi huku Kagera wakijiongezea alama tatu muhimu wakifikisha alama 43. #SIMBASC https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
Kagere na Okwi wameifunga magoli matatu kila mmoja huku Hassan Dilunga na Clatous Chama wakifunga moja moja.
Simba SC yakwaa kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania kwa kishindo kikubwa, yaitandika Coastal Union 8-1 uwanja wa Uhuru huku Okwi na Kagere wakifunga hat-trick kila mmoja na Yanga SC yawasili Mara tayari kuivaa Biashara United. Kwa hayo na mengine mengi ungana na Fatma Abdallah Chikawe ndani ya Mshikemshike Viwanjani.
HATRICK ya KAGERE na OKWI Wakabidhiwa Mipira Waionyoosha Coastal Washambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Okwi na Messy Kagere wameweka rekodi ya kufunga mabao sita yaani hat trick mbili ndani ya mechi moja. Wachezaji hao wote wenye asili ya Uganda kwa kuwa Okwi ni Mganda na Kagere ni Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, wamefunga bao hizo sita wakati Simba ikiitwanga Coastal Union kwa mabao 8-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mabao hayo, yanamfanya Kagere kufikisha mabao 20 msimu katika ligi kuu akifikia rekodi ya mabao 20 ya Okwi msimu uliopita lakini akibakiza bao moja kufikia idadi ya mabao 21 aliyofunga Amissi Tambwe msimu wa 2015/16 akiwa mfungaji bora. Kwa mabao hayo 14, Okwi naye amemfikia nahodha wake John Bocco aliyekuwa benchi katika mechi ya leo akishuhudia 'vijana wake" wakiwagaragaza Wagosi wa Kaya. Mabao mengine yalifungwa na Hassan Dilunga na Cleotus Chama raia wa Zambia na kuifanya Simba iandike ushindi huo mnono zaidi. Kwa ushindi wa leo, Simba imefikisha pointi 81 na kupaa kileleni ikiwaacha Yanga wenye pointi 80 waliokuwa wamekaa kileleni kwa muda mrefu zaidi. Yanga wamecheza 34 huku Simba wakiwa wamefikisha mechi 31 baada ya kucheza mechi yao ambayo wametoa kipigo kikali kwa Wagosi wa Kaya. #SIMBAVsCOASTALUNION https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho