SIMBA YAIFUMUA MAJI MAJI 5-0 | Walivyotua Uwanja wa Mkapa
SIMBA YAIFUMUA MAJI MAJI 5-0 | Walivyotua Uwanja wa Mkapa

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MABINGWA watetezi, Simba SC wamesonga mbele michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Maji Maji ya Songea usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC katika mchezo wa leo yamefungwa na beki mzawa Gardiel Michael dakika ya tatu, mshambuliaji Mkongo Chris Mugalu dakika ya sita, beki Mzanzibari Ibrahim Ame dakika ya 60, mshambuliaji Mrwanda Meddie Kagere dakika ya 78 na kiungo kutoka Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 90. HABARI MPYA DAILY:https://bit.ly/3c3bEDc HABARI ZA MICHEZO: https://bit.ly/2TAgnWx HABARIZA WASANII: https://bit.ly/2X2f84R HABARI ZA SIASA: https://bit.ly/36r0xCW Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars



Cameroon 4 - 1 Mozambique: All Goals & Extended Highlights
Cameroon 4 - 1 Mozambique: All Goals & Extended Highlights

Cameroon 4 - 1 Mozambique: All Goals & Extended Highlights خلاصه بازی و همه گلها: کامرون مقابل موزامبیک, Résumé du match et tous les buts: Cameroun vs Mozambique, Muhtasari wa mchezo na malengo yote: Kameruni dhidi ya Msumbiji, Resumo do jogo e todos os gols: Camarões x Moçambique, Spelopsomming en alle doele: Kameroen teen Mosambiek, ملخص المباراة وجميع الأهداف: الكاميرون ضد موزمبيق, 比賽總結和所有進球:喀麥隆vs莫桑比克, 경기 요약 및 모든 골 : 카메룬 vs. 모잠비크, ゲームの概要とすべての目標:カメルーン対モザンビーク, Ukufingqwa komdlalo nayo yonke imigomo: ICameroon vs. Mozambique, Итоги игры и все голы: Камерун - Мозамбик, -=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=- #OsMambas #CAN202Q #Afcon2021q #Cameroun #Mozambique #CMRMOZ #TOTALAFCON2021Q #AllezLesLions #ROADTOAFCON2022 -=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=- You can watch the similar videos on the below link: https://www.youtube.com/channel/UCiMamE_9lgNlDu3TUQkaGYg?sub_confirmation=1 -=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=- Please Like, Share & Subscribe For More...



SIMBA TV 31/8/2019: Tumeufunga ukurasa wa Kimataifa, tunaanza majukumu ya Kitaifa
SIMBA TV 31/8/2019: Tumeufunga ukurasa wa Kimataifa, tunaanza majukumu ya Kitaifa

SIMBA TV EPISODE 20: Tunakuonesha jinsi tulivyomalizana na majukumu ya Kimataifa kwa kukosa bahati na kutolewa kwenye Ligi ya mabingwa Afrika kwa kutoka sare ya bao 1-1 na UD Songo ya Msumbiji. Lakini pia utashuhudia jinsi ambavyo safari ya majukumu ya Kitaifa ilivyoanza kwa kuichapa JKT Tanzania. Simba SC #NguvuMoja



Ona Aussems aibua jambo Simba.
Ona Aussems aibua jambo Simba.

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amefurahi na kusema wachezaji wake walicheza kama watoto, licha ya ushindi wa mabao 3-1 ilioupata timu yake dhidi ya JKT Tanzania juzi Uwanja wa Uhuru,  Dar es Salaam. Simba ilipata ushindi huo katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Aussems alisema anaamini kikosi chake kilistahili kushinda idadi kubwa zaidi ya mabao katika mchezo huo, lakini kutokana na umakini mdogo wa wachezaji wake wakapata matokeo waliyopata. “Tumepata ushindi wa mabao 3-1, matokeo ambayo sijaridhishwa nayo kutokana na aina ya wachezaji nilioa nao kikosini, tulitakiwa kufunga mabao manne hadi sita lakini makosa ya kitoto waliyofanya yamesababisha tupate tulichopata,” alisema. Alipoulizwa sababu ya kuwatumia wachezaji ambao baadhi wamekuwa wakianzia benchi alijibu kuwa alifanya hivyo kutokana na wengine kusumbuliwa na majeraha. Aussems alisema wanaanza upya na kuachana na matokeo ya nyuma baada ya timu yake kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya awali na  timu ya UD Songo ya Msumbiji. Wekundu hao walifungashiwa virago, baada ya kulazimisha suluhu ugenini jijini Beira, kisha kutoka sare ya bao 1-1 , Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matokeo hayo yaliifanya UD Songo isonge mbele kwa faida ya bao la ugenini. Aussems alisema amewatengeneza wachezaji wake kisaikolojia ili wasahau yaliyopita na kuwekeza akili zao kuhakikisha wanapata matokeo mazuri Ligi Kuu na kutetea ubingwa wao. “Tulihuzunika kwani haikuwa rahisi kupokea matokeo yale, lakini kwenye mpira lolote linaweza kutokea, hata hivyo tumesahau yaliyopita na sasa macho na nguvu zetu zote tumehamishia Ligi Kuu,” alisema. Simba inashika nafasi ya pili wa Ligi Kuu, ikiwa na  pointi tatu, sawa na Lipuli, Azam, Kagera Sugar, Namungo, Mwadui, Polisi Tanzania na Ruvu Shooting, zikitofautiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.



SIMBA KUTOLEWA: SAbabu 5 za kiufundi hizi hapa-Aussems/ Kahata/ Shiboub.
SIMBA KUTOLEWA: SAbabu 5 za kiufundi hizi hapa-Aussems/ Kahata/ Shiboub.

#SimbaSC #UdSongo #SoccerData Wikiendi hii Simba ilicheza mechi ya Kimataifa dhidi ya UD Do Songo ya Nchini Msumbiji, ikiwa ni mechi ya marudiano katika mashindano ya ligi ya mabaingwa Afrika hatua ya mchujo yaani preliminary stage. Katika matokeo ya awali Simba ilitoka sare tasa, hivyo katika mchezo wa marudiano Simba ilihitaji ushindi wowote ule. Simba imetoka sare pacha ya goli moja kwa moja, na kuilazimisha Simba kutupwa nje ya mashindano. Ud Songo wamepita hatua hii na sasa watakutana na FC Platnum kwa faida ya goli la ugenini. Channeli inakuletea Uchambuzi wa kiufundi wa mechi hii, hapa utapata kujua mbinu za walimu wa timu zote mbili, wapi kulikuwa na udhaifu, vikosi vya timu zote mbili, na ni kwanini Simba ilipata matokeo iliyoyapata, walikwama wapi kimbinu na kimkakati. Ungana na chaneli hii sasa kwa KU SUBSCRIBE NA KISHA bofya alama ya Kengele, kufanya hivyo kutakufanya usikose video zingine za kiuchambuzi zenye lengo la kuweka mambo sawa kiufundi.



SHABIKI WA SIMBA AMWAGA MACHOZI BAADA YA TIMU YAO KUTOLEA NYUMBANI NA UD SONGO YA MSUMBIJI
SHABIKI WA SIMBA AMWAGA MACHOZI BAADA YA TIMU YAO KUTOLEA NYUMBANI NA UD SONGO YA MSUMBIJI

All sports, all the time, all Tanzania, Africa and the rest of the world. All sporting previews, results, reviews, breaking news, transfers and updates. Football, athletics, track and field, motorsport, basketball, vollyeball and other sporting news.



UD Songo Kutua Dar ijumaa,Simba hakuna kulegeza kamba wako fiti kila idara.
UD Songo Kutua Dar ijumaa,Simba hakuna kulegeza kamba wako fiti kila idara.

ZIKIWA zimebaki takribani siku nne kabla ya Simba kuivaa UD do Songo kutoka Msumbuji, rekodi zinaonyesha kuwa Simba wana asilimia kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Jumapili ya wiki hii. Tangu msimu uliopita, Simba katika michuano ya kimataifa haijapoteza mchezo wowote waliocheza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambao ndiyo uwanja wanaoutumia kwa mechi zao za nyumban Katika mchezo huo wa marudiano, Simba inaingia ikiwa na rekodi ya kushinda michezo mitano ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita kati ya sita iliyocheza hapo ambapo mmoja pekee ilitoka suluhu. Michezo ambayo Simba ilibuka na ushindi walipocheza nyumbani kwenyeUwanja wa Taifa ni; Simba 4-1 Mbabane Swallows, Simba 3-1 Nkana, Simba 3-0 JS Saoura, Simba 1-0 Al Ahly na Simba 2-1 AS Vita Club. Ule wa suluhu ni dhidi ya TP Mazembe. Simba na UD Songo zilipokutana Msumbiji, matokeo yalikuwa suluhu jambo ambalo linaipa nafasi kubwa Simba kusaka ushindi ili isonge hatua inayofuata.



UD SONGO Wamfanyia Kitu Mbaya CHAMA ,simba, “Katika mchezo huo Chama hakufanikiwa kufanya vizuri "
UD SONGO Wamfanyia Kitu Mbaya CHAMA ,simba, “Katika mchezo huo Chama hakufanikiwa kufanya vizuri "

#chama #simbasc #udsongo KIUNGO wa Simba raia wa Zambia, Clatous Chama, Jumamosi iliyopita ilikumbana na balaa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo uliofanyika nchini Msumbiji.   Katika mchezo huo, Chama anadaiwa kupewa ulinzi mkali na wapinzani ili kuhakikisha hapati nafasi ya kuanzisha mashambulizi kama ambavyo alikuwa akifanya katika michuano hiyo msimu uliopita.   Akizungumza na DREAM ONLINE TV mmoja wa wachezaji wa Simba ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa, kama Chama katika mchezo huo angekuwa sawa basi wangepata ushindi.   “Tunamshukuru Mungu tumerudi salama japokuwa hatukupata ushindi lakini kazi ilifanyika, pia wapinzani wetu walijitahidi sana kuzijua mbinu zetu ambazo tumekuwa tukizitumia kupata ushindi.   “Katika mchezo huo Chama hakufanikiwa kufanya vizuri kutokana na ulinzi mkubwa aliokuwa amewekewa na wapinzani wetu hao, kwani kila alivyokuwa akishika mpira tayari kuna watu wawili wanamzunguka jambo ambalo lilisababisha asifanye vizuri kama tulivyotarajia.   “Hata hivyo ni matumaini yetu ni kuwa kocha atakuwa ameliona hilo na atalifanyia kazi ili katika mchezo wa marudiano tutakaocheza hapa nchini tuweze kupata ushindi,” alisema mchezaji huyo.   Alipoulizwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems alisema: “Mchezo huo ulikuwa wa wazi na tulikuwa tukishambuliana kwa zamu na zaidi wapinzani wetu walijitahidi sana kuhakikisha wanadhibiti sehemu yetu ya kiungo ili viungo wetu wasipate nafasi ya kutengeneza nafasi za kufunga, hata hivyo katika mchezo wa marudiano tutahakikisha tunafanya vizuri katika uwanja wetu wa nyumbani.”




« Previous Next »


Popular Tags

#Zlatan Ibrahimovi  #Cristiano Ronaldo  #Cleveland Cavaliers  #New York Knicks  #Michael Jordan  #Gareth Bale  #Shot Goals  #Paul Pogba  #Football Defensive Skills  #Allen Iverson  

Popular Users

#JasonDufner  #elonmusk  #hunterpence  #TheEllenShow  #josecanseco  #katyperry  #jtimberlake  #katzm  #tigerwoods  #BellaTwins  #iamsrk  #TheNotoriousMMA  #RobbieSavage8  #realDonaldTrump