Singida BS imefanya 'come-back' na kushinda 4-2 dhidi ya Azam FC baada ya kutanguliwa 2-0, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Azam wametangulia kupata magoli yao kupitia kwa Feisal Salum Feitoto kwa penati, na Zidane Sereri, lakini Singida wakaanza kuyalipa kupitia kwa Emmanuel Keyekeh, James Mwashinga na Jonathan Sowah aliyefunga mawili ya mwisho. Singida BS pia walikosa penati iliyopigwa na Emmanuel Keyekeh na kuokolewa na golikipa Zuberi Foba. Tazama magoli yote na penati ...