UGANDA1-0 TANZANIA BARA: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (SEMI FINAL 2 CECAFA SENIOR CHALLENGE 17/12/2019) by @Azam TV - Post Details

UGANDA1-0 TANZANIA BARA: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (SEMI FINAL 2 CECAFA SENIOR CHALLENGE 17/12/2019)

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara (The Kilimanjaro Stars) imeshindwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA Kombe la Chalenji baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wa michuano hiyo Uganda (The Cranes). Kilimanjaro Stars katika mchezo huo walicheza kwa tahadhari kubwa lakini bahati haikuwa upande wao kwani mnamo dakika ya 86 ya mchezo Uganda walifanikiwa kupata bao lililofungwa na Fahad Bayo na kutinga hatua ya fainali. Uganda itacheza fainali dhidi ya Eritrea ambayo leo imewavua ubingwa Kenya (The Harambee Stars) katika moja ya mechi ya kushangaza na kusisimua ikipata ushindi wa mabao 4-1.

Similar Posts!

USIKU WA VITASA | Karim Mandoga Vs Mada Maugo (TKO) - 11/04/2024
USIKU WA VITASA | Karim Mandoga Vs Mada Maugo (TKO) - 11/04/2024

Kwa TKO raundi ya sita, Mada Maugo amemkalisha Karim Mandonga.

Mashujaa FC 1-1 (6-5) Simba SC | Penati | CRDB Bank Federation Cup - 09/04/2024
Mashujaa FC 1-1 (6-5) Simba SC | Penati | CRDB Bank Federation Cup - 09/04/2024

Tazama mikwaju yote ya penati iliyopigwa kwenye mchezo CRDB Bank Federation Cup kati ya Mashujaa FC dhidi ya Simba SC. Simba imetolewa kwa jumla ya penati 6-5 Waliopiga kwa upande wa Simba ni Mohamed Hussein, Israel Mwenda, Freddy Michael Koublan, Willy Onana, Mzamiru Yassin, Ladack Chasambi, Sadio Kanoute Waliopiga kwa upande wa Mashujaa ni Zuberi Dabi, Samson Madeleke, Masinda, Idrissa Stambuli, Adam Adam, Mpoki Mwakinyuke, Baraka Mtui

Yanga kupeleka malalamiko CAF yaliyojiri mechi yao na Mamelodi Sundowns
Yanga kupeleka malalamiko CAF yaliyojiri mechi yao na Mamelodi Sundowns

“Kama klabu lazima tuoneshe kwamba kuna namna ambavyo hatujaridhishwa na kile ambacho kimetokea katika mchezo ule” sehemu ya maneno ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe akizungumzia hatua ambazo timu hiyo imepanga kuzichukua juu ya yale yaliyojiri katika dimba la Loftus kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

MSHIKESMSHIKE VIWANJANI - 03/04/2024
MSHIKESMSHIKE VIWANJANI - 03/04/2024

Tazama taarifa mbalimbali za maandalizi ya Simba na Yanga SC kuelekea mechi zao za marudiano za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Afrika.

MSHIKEMSHIKE VIWANJANI 01/04/2024
MSHIKEMSHIKE VIWANJANI 01/04/2024

Tazama kipindi cha Mshikemshike Viwanjani ambacho kimekusanya habari mbalimbali ikiwemo taarifa ya Rais wa Yanga, Hersi Said akizungumzia mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo. Mashabiki wa Yanga wameanza safari ya kwenda Mamelodi

Azam FC 2 -1 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 17/03/2024
Azam FC 2 -1 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 17/03/2024

DAR DERBY: Yanga SC imeangukia pua kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam FC, katika #DarDerby iliyopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Yanga imetangulia kupata bao kupitia kwa Clement Mzize dakika ya 10 kabla ya Azam kuchomoa dakika ya 19 kwa goli la Gibril Sillah na kisha Feisal Salum akafunga la ushindi dakika ya 51.

Magoli | Azam FC 2-1 Yanga SC | NBC Premier League 17/03/2024

Simba 2-0 Mashujaa | Highlights | NBC Premier League 15/03/2024
Simba 2-0 Mashujaa | Highlights | NBC Premier League 15/03/2024

Clatous Chama amefunga magoli mawili muhimu dakika ya 57 na 73, Simba ikipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Mashujaa FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa #AzamComplex, Chamazi .