Content removal request!


UGANDA1-0 TANZANIA BARA: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (SEMI FINAL 2 CECAFA SENIOR CHALLENGE 17/12/2019)

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara (The Kilimanjaro Stars) imeshindwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA Kombe la Chalenji baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wa michuano hiyo Uganda (The Cranes). Kilimanjaro Stars katika mchezo huo walicheza kwa tahadhari kubwa lakini bahati haikuwa upande wao kwani mnamo dakika ya 86 ya mchezo Uganda walifanikiwa kupata bao lililofungwa na Fahad Bayo na kutinga hatua ya fainali. Uganda itacheza fainali dhidi ya Eritrea ambayo leo imewavua ubingwa Kenya (The Harambee Stars) katika moja ya mechi ya kushangaza na kusisimua ikipata ushindi wa mabao 4-1.