Dream Online Tv's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
#mediekagere #simbasc #mbinu MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba, ametoa tahadhari kwa wachezaji wenzake akisema kwamba hawatakiwi kuwachukulia kirahisi wapinzani wao UD do Songo. Simba itamenyana na UD Songo kwenye mchezo wa marudio kati ya Agosti 23-25 jijini Dar baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Msumbiji. Msimu uliopita kwenye michuano ya kimataifa, Kagere alitupia mabao sita ana kazi ya kufanya pamoja na wachezaji wake kwenye mchezo wa marudio ili kusonga mbele. “Kuelekea mchezo wa marudio tunatakiwa kuwa makini na kuchukulia kwa uzito mkubwa pambano ambalo tutachezwa kwani mashabiki pamoja na uongozi unahitaji matokeo,
PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hesabu kubwa ni mchezo wake wa ngao ya jamii dhidi ya #AzamFC utakaopigwa Jumamosi uwanja wa Taifa #Aussems amesema mpango wa mechi ya kimataifa dhidi ya UD do Songo ameuweka kando kwa muda. "Hesabu kubwa ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam ambao utaanza kabla ya marudiano na UD do Songo. "Nikimaliza kucheza na Azam nitakuwa na muda wa kuifikiria UD do Songo na nina amini utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani," amesema. Mchezo wa kwanza wa kimataifa hatua ya awali #Simba ililazimisha sare dhidi ya UD Songo ya Msumbiji hivyo wana kazi kupata matokeo mechi ya marudiano ili kusonga mbele inayotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25.
UONGOZI wa #Simba umesema kuwa kwenye mchezo wa marudio wa kimataifa dhidi ya UD Songo, unaotarajiwa kuchezwa uwanja wa Taifa itakuwa ngumu kwa wapinzani wao kutoka salama kwani wamejipanga kufunga hesabu jumlajumla. Simba itarudiana na #UDSongo ya Msumbiji kati ya Agosti 23-25 ikiwa ni mchezo wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwenye mchezo wa kwanza ambao ulichezwa uwanja wa Beira, Simba ililazimisha sare ya kutofungana hivyo ili kusonga mbele wana kazi ya kushinda kwenye mchezo huo. Ofisa Habari wa Simba, #HajiManara amesema kuwa haikuwa kazi nyepesi kwa kikos kufika hapo ila watatumia nafasi ya kuwa nyumabni kushinda. "Haikuwa malengo yetu kushindwa kupata matokeo ila kwa hatua ambayo tumefikia tuna nafasi ya kushinda tukiwa nyumbani hivyo muda ni wetu wa kufanya yetu kimaaifa. "Mashabiki wa Simba tujiandae na kazi hii kubwa kwa ajili ya Taifa, kikubwa ni sapoti na imani yetu ni kwamba hatatoka mtu salama pale Taifa,"
#PATRICK Aussems,raia wa Ubelgiji ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa matokeo waliyoyapata jana kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya UD Songo sio mabaya kwani bado wana nafasi ya kupata ushindi. Simba jana ilicheza mchezo wa kwanza wa kimataifa kwenye hatua ya awali dhidi ya UD Songo, uwanja wa Beira nchini Msumbiji mpaka dakika 90 kukamilika ubao ulikuwa unasoma 0 kwa UD Songo na Simba pia. "Tumefanya kitu kizuri kutoruhusu bao, juhudi kubwa za wachezaji wangu pamoja na juhudi za wapinzani zimeshindwa kuzaa matunda hivyo tunajiaanda kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio. "Mchezo wetu wa marudio Dar, tuna nafasi ya kufanya vizuri, mashabiki watupe sapoti tutapambana," amesema. Simba itarudiana na UD Songo kati ya Agosti 23-25 jijini Dar, uwanja wa Taifa.
#taifastars #harambeestars TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo imesonga mbele hatua inayofuata ya michuano ya Chan baada ya kushinda mbele ya Kenya. Dakika tisini zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu na kuamuliwa kwenda kwenye mikwaju ya penalti. Tanzania imeshinda kwa penalti 4 huku Kenya ikipachika penalti 1 .Mlinda mlango Juma Kaseja leo amepangua penalti mbili huku kwa upande wa Stars wapachika mabao wakiwa ni Erasto Nyoni,Paul Godfrey, Gadiel Michael na msumari wa mwisho ukikomelwa na Salim Aiyee. Mchezo unaofuata Kwa Stars ni dhidi ya Sudan katika hatua ya pili kabla ya kufuzu michuano hii moja Kwa moja.