Content removal request!


ONA HII MBELGIJI WA SIMBA AANDAA DAWA HII HAPA YA KUWAMALIZA WABAYA WAO KIMATAIFA DAR.

#PATRICK Aussems,raia wa Ubelgiji ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa matokeo waliyoyapata jana kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya UD Songo sio mabaya kwani bado wana nafasi ya kupata ushindi. Simba jana ilicheza mchezo wa kwanza wa kimataifa kwenye hatua ya awali dhidi ya UD Songo, uwanja wa Beira nchini Msumbiji mpaka dakika 90 kukamilika ubao ulikuwa unasoma 0 kwa UD Songo na Simba pia. "Tumefanya kitu kizuri kutoruhusu bao, juhudi kubwa za wachezaji wangu pamoja na juhudi za wapinzani zimeshindwa kuzaa matunda hivyo tunajiaanda kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio. "Mchezo wetu wa marudio Dar, tuna nafasi ya kufanya vizuri, mashabiki watupe sapoti tutapambana," amesema. Simba itarudiana na UD Songo kati ya Agosti 23-25 jijini Dar, uwanja wa Taifa.