Dream Online Tv's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
HIZI NDIZO Sababu kuu tatu za simba kutolewa na UD SONGO Klabu bingwa afrika,ZINAUMIZA/ POLENI SIMBA
UD SONGO WALIISHINDA SIMBA KWA KUTUMIA SILAHA ZA SIMBA, WAKATI WA KUNYANYUKA NA KUSONGA MBELE NI SASA
#chama #simbasc #udsongo KIUNGO wa Simba raia wa Zambia, Clatous Chama, Jumamosi iliyopita ilikumbana na balaa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo uliofanyika nchini Msumbiji. Katika mchezo huo, Chama anadaiwa kupewa ulinzi mkali na wapinzani ili kuhakikisha hapati nafasi ya kuanzisha mashambulizi kama ambavyo alikuwa akifanya katika michuano hiyo msimu uliopita. Akizungumza na DREAM ONLINE TV mmoja wa wachezaji wa Simba ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa, kama Chama katika mchezo huo angekuwa sawa basi wangepata ushindi. “Tunamshukuru Mungu tumerudi salama japokuwa hatukupata ushindi lakini kazi ilifanyika, pia wapinzani wetu walijitahidi sana kuzijua mbinu zetu ambazo tumekuwa tukizitumia kupata ushindi. “Katika mchezo huo Chama hakufanikiwa kufanya vizuri kutokana na ulinzi mkubwa aliokuwa amewekewa na wapinzani wetu hao, kwani kila alivyokuwa akishika mpira tayari kuna watu wawili wanamzunguka jambo ambalo lilisababisha asifanye vizuri kama tulivyotarajia. “Hata hivyo ni matumaini yetu ni kuwa kocha atakuwa ameliona hilo na atalifanyia kazi ili katika mchezo wa marudiano tutakaocheza hapa nchini tuweze kupata ushindi,” alisema mchezaji huyo. Alipoulizwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems alisema: “Mchezo huo ulikuwa wa wazi na tulikuwa tukishambuliana kwa zamu na zaidi wapinzani wetu walijitahidi sana kuhakikisha wanadhibiti sehemu yetu ya kiungo ili viungo wetu wasipate nafasi ya kutengeneza nafasi za kufunga, hata hivyo katika mchezo wa marudiano tutahakikisha tunafanya vizuri katika uwanja wetu wa nyumbani.”
IKICHEZA kwa kujiamini na mbinu za hali ya juu, juzi Jumamosi Simba ililazimisha suluhu ugenini dhidi ya wenyeji, UD Songo ya Msumbiji. Katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Beira, Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisisitiza kwamba; “Tunakwenda kumaliza kazi Dar.” Simba iliandika rekodi ndani ya msimu mpya baada ya kutoruhusu bao lolote ikianzia mashindano hayo makubwa ugenini. Msimu uliopita kwenye hatua ya awali Simba ilianzia nyumbani dhidi ya Mbabane ikashinda 4-1, ugenini ikashinda mabao 4-0. Baada ya hapo katika mechi zote ilizocheza ugenini ikaruhusu mabao mengi. Katika mchezo wa jana Simba ilionekana kucheza kwa kujiamini huku safu ya ulinzi ikifanya kazi ya ziada. Ndani ya dakika 45 za kwanza Simba ilipiga mashuti matatu ambayo hayakuwa na madhara lakini mengine mawili nusura yawaamshe mashabiki kwani kipa alipangua yakawa kona. Wekundu hao walipata kona nne za haraka huku wakionekana kutawala zaidi eneo la katikati na kuwalazimisha wenyeji kupiga pasi ndefu ambazo hata hivyo walionyesha udhaifu mkubwa kwenye umaliziaji kwani walikuwa wakipaisha au kupiga pasi fyongo ambazo zilikuwa mboga kwa Benno Kakolanya. UD Songo walicheza mpira wa kuvizia kipindi cha pili lakini wakadhibitiwa na Nyoni na Wawa ambao walionekana kujiamini. Shiboub ambaye ni raia wa Sudan katika mechi jana alitawala kiungo na kuziba mianya mingi ya wenyeji kuwafikia mabeki wa Simba. Mkude muda mwingi alikuwa akiinasa mipira, kuidhibiti na kumpa Chama ambaye kazi yake ilikuwa kusambaza tu. Kwa mujibu wa kocha na viongozi wa Simba, uwanja uliochezwa mechi hiyo wa Campo Do Ferroviario Da Beira ulikuwa chakavu sana na haukuruhusu kucheza kiwango chao ingawa suluhu bado inawabeba. Aussems alisisitiza kwamba wana nafasi kubwa ya kushinda Dar es Salaam kwenye mechi ya marudiano na kusonga mbele na hawana wasiwasi. “Ulikuwa mchezo wa wazi, walikuwa wakijaribu kufunga na kwetu ilikuwa hivyo, jambo muhimu hatujaruhusu goli. Mchezo wa marudiano utakaochezwa Dar ni muhimu, kwa ushangiliaji wa mashabiki wetu na uwanja mzuri nafikiri tutafanya vizuri,” alisema Kocha Aussems.
#BENOKakolanya mlinda mlango mpya wa Simba ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwli akitokea Yanga amemkosha, Patrick #Aussems kutokana na uwezo wake. Kakolanya alianza kwenye mchezo wa kwanza wa kimataifa hatua ya awali dhidi ya UD Songo nchini Msumbiji na hakuruhusu nyavu zake kuguswa licha ya kukumbwa na hatari nyingi langoni mwake. Aussems amesema: “Kakolanya anafanya vizuri, sina wasiwasi tena kama ilivyokuwa msimu uliopita nilivyokuwa nikipata taabu pindi Manula akiumia. “Mechi zote alizocheza amefanya vizuri kwa hiyo ni matumaini yangu kuwa kadiri siku zinavyoenda atakuwa bora zaidi na atatoa changamoto kubwa #Manula,"