Shabiki wa Klabu ya Soka ya Simba Bwana Ramadhan Mohamed ambaye alikwenda Dar es Salaam akitokea Jijini Mbeya kwa miguu ili ashuhudie mchezo wa robo fainali ya #CAFCL kati ya Simba SC dhidi ya TP Mazembe kutoka DRC, leo amekutana na viongozi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na sekretarieti ya Klabu ya Soka ya Simba ambapo amehaidiwa kugharamiwa na klabu ya Simba kwenda Lubumbashi nchini DRC, kwaajili ya kuangalia mchezo wa marudiano kati ya TP Mazembe dhidi ya Simba SC ambao utachezwa Jumamosi hii. #NguvuMoja #SimbaSc #YesWeCan #HajiManara