KUTOKA MISRI: Kikosi cha Simba kilichopo Misri, katika maandalizi ya msimu mpya wa NBC Premier League na mashindano ya kimataifa, kimecheza mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Carabat FC, ambapo Mnyama ameshinda magoli 2-0. Goli la kwanza lilifungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Mohammed Bajaber huku goli la pili likifugwa kipindi cha pili na Jonathan Sowah. Wachezaji wote wawili wamesajiliwa msimu huu. #Simba #KambiYaSimba
Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, amesema kikosi chake kiko tayari kwa mechi ya pili ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane ya Morocco huku akisisitiza kuwa wachezaji wake wameshajifunza kupitia maumivu ya dakika 20 za kwanza kule Morocco. Akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar, Fadlu amesema: “Ndiyo, tulikuwa tumejiandaa kikamilifu kwa mechi ya kwanza. Tulikuwa tumepanga kila kitu kiufundi na kimkakati, lakini jambo kubwa zaidi lilikuwa kuwapa wachezaji uzoefu wa dakika zile 20 za mwanzo kwa sababu unaweza kuwa na mpango mzuri lakini hali halisi ya uwanja na mazingira ya fainali huwezi kuifundisha darasani. Lazima waishi nayo, wapitie, na wakue kupitia hilo.” Katika mechi wa kwanza iliyochezwa Morocco, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-0. Hata hivyo, Fadlu anaamini kuwa kikosi chake sasa kiko tayari kwa pambano la marudiano, licha ya mchezo huo kuhamishiwa Zanzibar badala ya uwanja wao wa nyumbani wa Benjamin Mkapa. #samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama #Shot #mamelodisundowns #alahlytv #alahlysc #miraj
Yanga imeichakaza Stand United kutoka Championship mabao 8-1, manne yakitoka kwa Stephane Aziz Ki.... ukiwa ni mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho la CRDB Bank uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Magoli mengine yametoka kwa Clatous Chama aliyefunga mawili, Nickson Kibabae goli la pili na Kennedy Musonda goli la nane..... Goli la kufutia machozi kwa Stand United limefungwa na Msenda Senda dakika ya 49.
Yanga imeichakaza Stand United kutoka Championship mabao 8-1, manne yakitoka kwa Stephane Aziz Ki.... ukiwa ni mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho la CRDB Bank uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Magoli mengine yametoka kwa Clatous Chama aliyefunga mawili, Nickson Kibabae goli la pili na Kennedy Musonda goli la nane..... Goli la kufutia machozi kwa Stand United limefungwa na Msenda Senda dakika ya 49. Haya hapa magoli yote tisa...
MZIZIMA DERBY | Ni sare ya 2-2 kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC, uliopigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Azam wametangulia kwa goli la Gibril Sillah dakika ya 01, kabla ya Elie Mpanzu kusawazisha dakika ya 25 na Abdulrazak Hamza kuongeza la pili dakika ya 76. Nyota wa mchezo ni ‘Super Sub’, Zidane Sereri ndiye aliyeweka mambo sawa kwa kuifungia Azam FC bao la kusawazisha dakika ya 88, kwa assist ya aina yake kutoka kwa Feisal Salum Feitoto.