Leo Machi 6,2024 Mnyama Simba anashuka Dimba la Jamhuri Morogoro kumenyana na Wajelajela Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ,Saa 10:00 jioni.
Simba SC imechezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons, katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la Jamhuri, Morogoro. Magoli yote mawili ya Tanzania Prisons yamefungwa na Samson Mbangula dakika ya 45 na 62 huku goli pekee la Simba likipatikana dakika ya 89 kupitia kwa Fabrice ngoma. Tazama Highlights....
Leo Februari 17,2024 KMC FC inashuka Dimba la Jamhuri Morogoro kuikaribisha Yanga SC katika mchezo wa ligu kuu ya NBC,Saa 10:00 Jioni. Kaa karibu na Mpenja TV kupata taarifa zote za kabla na baada ya mchezo huo.
Leo ndio Leo 🔥 ndani ya Mkoa wa Morogoro Wadau na wapenzi wa Soka Watashuhudia Burudani safi ya mpira wa Miguu katika Dimba la Jamhuri 🏟.. Ni Mchezo wa Hisani WAPE TABASAMU 2023 kati ya TEAM KIBWANA SHOMARI Vs TEAM DICKSON JOB ⏰ Kuanzia Saa 08:00 Mchana JE, Unadhani nani ataibuka Mbabe 😊⁉️ Endelea Kuwa karibu na Mpenja Tv kwa Updates Zaidi.
Team Job ambayo iko chini ya beki Dickson Job wa Yanga imeibuka na ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Team Kibwana iliyo chini ya Kibwana Shomary baada ya sare ya 2-2 katika muda wa kawaida, ukiwa ni mchezo wa hisani kusaidia afya ya uzazi ikienda kwa jina la #WapeTabasamu . Yamefungwa magoli manne na wachezjazi wawili katika muda wa kawaida.... Wachezaji hao ni Abdul Suleiman Sopu akiifungia Team Kibwana magoli mawili dakika ya 23 na 50 huku Saimon Msuva akichomoa magoli yote mawili dakika ya 74 na 80. Mechi imepigwa kwenye Dimba la Jamhuri, Morogoro. Shuhudia hapa magoli yote na mikwaju ya penati.
Leo tarehe 22/06/2023 imetolewa tarehe rasmi ya Mchezo wa Wape Tabasamu 2023 ambao utapigwa Mkoani Morogoro ukikutanisha Timu Kibwana Dhidi ya Timu Dickson Job kwenye Uwanja wa Jamhuri. Dhumuni kubwa la Mchezo huo ni Uzazi Salama kwa Kizazi Bora. Kocha wa Timu Kibwana ni George Ambangile huko Kocha wa Timu Job akiwa ni Ally Kamwe