Hii ni sehemu ya kipindi cha Dakika 90 kilichoruka Jumatatu Desemba 17 Azam Sports 2 ambapo wachambuzi wetu Charles Abel na Thobias Sebastian wameyaweka wazi makossa yaliyofanywa na wachezaji wa Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana FC. Fuatilia mjadala huu.
Kuna mwengi yametikisa michezoni wiki hii lakini kurasa za mwisho za magazeti ambazo huandika habari za michezo, zimetoa kipaumbele zaidi kwa habari ya usajili ndani ya klabu ya Yanga, ambao wametumia dirisha dogo kumnasa kiungo Haruna Moshi Boban. Taarifa nyingine iliyopewa uzito ni kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Nkana FC dhidi ya Simba SC unaopigwa leo Desemba 15, 2018 nchini Zambia. Ndani ya Studio Philip Cyprian yuko na wanahabari nguli wa michezo, wanafanya uchambuzi na mjadala kuhusu yaliyopewa uzito kwenye kurasa hizo. Vilevile tumetembelea vibanda vya magazeti na kuzungumza na wafuatiliaji wa habari za michezo magazetini, wengi wakiwa ni mashabiki wa soka. Kipindi hiki ni kila Jumamosi saa 3:30 asubuhi Azam Sports 2.
Ni mjadala kuhusu yanayojiri katika ligi daraja la kwanza Tanzania Bara, ambapo baada ya ushindi wa Biashara United ugenini, Mkuu wa mkoa wa Mara ametoa tamko. Mjadala huu umefanyika katika kipindi cha Sports AM ambacho hukujia kila Jumamosi na Jumapili saa 1:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi kupitia Azam Sports 2 ambapo mjadala wa leo Jumapli uliongozwa na Pascal Kabombe