Baada ya Simba Kufungwa 2-0 na JS SOURA, Hesabu Zaibeba Caf
Baada ya Simba Kufungwa 2-0 na JS SOURA, Hesabu Zaibeba Caf

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MAKOSA ya safu ya ulinzi ya Simba, jana yaliigharimu timu hiyo na kujikuta ikipigwa mabao 2-0 na JS Saoura nchini Algeria lakini wamesisitiza kwamba nguvu zote sasa ni kwa AS Vita Jumamosi. Simba sasa imeelekeza nguvu zote kwenye mechi ya AS Vita ili kucheza karata ya mwisho ya kutafuta nafasi ya kufuzu robo fainali. Hesabu zinaibeba Simba kwani ikishinda mchezo huo itafi kisha pointi tisa na kusonga mbele. Kwenye mechi ya jana safu ya ulinzi ya Simba chini ya Paschal Wawa, Mohammed Tshabalala na Paul Bukaba haikuwa na uelewano mzuri jambo ambalo liliwapa Saoura nguvu ya kushambulia. Mabao ya wenyeji yalifungwa na Yahya Sherrif kwa shuti la kiufundi huku la pili likipachikwa na Mohammed Amine kwa penalty. Amine alifanyiwa faulo na Bukaba ambaye kipindi cha kwanza nusura ajifunge alipokuwa akiokoa. Sasa Simba imeelekeza nguvu zake kwa mechi ya Jumamosi saa moja usiku kwenye Uwanja wa Taifa ambayo wamesisitiza kwamba hata kama Mwinyi Zahera wa Yanga atauza siri zao kwa Vita potelea mbali lakini ushindi lazima. Kocha wa Simba,Patrick Aussems amefunga ukurasa wa mchezo wa jana na kuanzia leo ni kazi moja tu huku mashabiki nao wakisisitiza kupambana. Zahera aliliambia Spoti Xtra kwamba; “Simba atamfunga Vita kwenye Uwanja wa Taifa na wanaweza kwenda robo fainali, lakini haiwezi kubeba ubingwa wa Afrika.” “Haina timu yenye uwezo huo. Lakini ni ukweli usiofi chika kwamba mimi Vita nitawapa mbinu za Simba kwavile wale ni rafi ki zangu na kocha wao ni bosi wangu kwenye timu ya Taifa. “Siwezi kuwafi cha, ila itakuwa ni mechi ngumu sana na nzuri,”alisema Zahera ambaye anadai kwamba Simba inamuombea mabaya kwenye Ligi Kuu na FA. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars



ZAHERA AAHIDI MAUMIVU KWA SIMBA MPAKA MWISHO WA MSIMU,BIGWA NI NANI? KATI YA AZAM FC, YANGA NA SIMBA
ZAHERA AAHIDI MAUMIVU KWA SIMBA MPAKA MWISHO WA MSIMU,BIGWA NI NANI? KATI YA AZAM FC, YANGA NA SIMBA

ZAHERA AAHIDI MAUMIVU KWA SIMBA MPAKA MWISHO WA MSIMU,BIGWA NI NANI? KATI YA AZAM FC, YANGA NA SIMBA



TANZANIA PRISONS 1-3 YANGA SC: FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 03/12/2018)
TANZANIA PRISONS 1-3 YANGA SC: FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 03/12/2018)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, leo wamefanya kweli Jijini Mbeya kwa kuichapa Tanzania Prisons jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Wenyeji Tanzania Prisons ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Jumanne Elifadhili, penati ambayo ilizua tafrani na kupelekea wachezaji watatu wa Yanga kupata kadi za njano. Yanga waliingia kivingine kipindi cha pili na kusukuma mashambulizi ya kasi hasa baada ya kuingia wachezaji wapya Matteo Anthony, Thabani Kamusoko na Amissi Tambe na kupata bao la kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Ibrahim Ajibu kwa mkwaju wa penati. SUPER SUB: Amissi Tambwe ameingia dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Juma Abdul, akasababisha penati iliyosababisha bao la kusawazisha, kisha akafunga mengine mawili dakika ya 85 na 90+2. Timu zote zililazimika kucheza pungufu baada ya Tanzania Prisons kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati, hali ikaonekana si shwari tena uwanjani na kupelekea vurugu ambazo zilizaa kadi nyekundu mbili, yaani moja kila upande. Mara baada ya mchezo wachezaji Mrisho Ngasa na Laurian Mpalile wamezungumza na kuomba radhi mashabiki kwa kitendo walichoonesha, huku Kocha Mwinyi Zahera akimwaga machozi.




« Previous Next »


Popular Tags

#Lionel Messi  #Football Defensive Skills  #Los Angeles Lakers  #Shaquille O'Neal  #LeBron James  #Shot Goals  #Best Ball Controls  #Ronaldinho  #Mesut Ozil  #Best Goalkeeper Saves  

Popular Users

#_BAnderson30_  #iamsrk  #Drake  #rolopez42  #BrunoMars  #hunterpence  #UKCoachCalipari  #BaileyLAKings  #blakegriffin23  #LilTunechi  #alexmorgan13  #rioferdy5  #BillGates  #Ky1eLong