Azam FC 2-0 Malindi SC | Highlights - Mechi ya Kirafiki 15/01/2021 by @Azam TV - Post Details

Azam FC 2-0 Malindi SC | Highlights - Mechi ya Kirafiki 15/01/2021

Timu ya Azam FC imeibuka na ushindi wa magoli mawili baada ya kuichapa Malindi FC katika mchezo wa kwanza wa kirafiki uliochezwa leo katika uwanja wa Mao Tse Tung, visiwani Zanzibar. Magoli mawili yote ya AZAM FC yalipatikana katika kipindi cha kwanza, ambapo Idd Seleman alifunga goli la kwanza katika dakika ya 17 ya mchezo, na goli la la pili likafungwa na Mudathir Mudathir dakika ya 45+2. AZAM FC itaendelea na mchezo wa pili wa kirafiki Jumamosi hii kwa kucheza na KMKM, na mchezo wa tatu utachezwa Jumatano ijayo dhidi ya kikosi cha Valantia Zanzibar (KVZ SC) Tufuatilie kwenye mitandao mingine ya kijamii:- ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamtvtz/ ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamsports2/ ►TWITTER: https://twitter.com/azamtvtz ►FACEBOOK: http://www.facebook.com/azamtvtz ►WEBSITE: http://www.azamtv.co.tz

Similar Posts!

Magoli | Yanga SC 3-0 Singida BS | NBC Premier League 22/05/2026
Magoli | Yanga SC 3-0 Singida BS | NBC Premier League 22/05/2026

Yamefungwa magoli matatu.... chuma mbili zikiwekwa kambani na Allan Okello na goli lingine likifungwa na Mudathir Yahya kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Hii ni Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.



Simba SC 4-0 TRA United | Highlights | CRDB Bank Federation Cup - 17/05/2026
Simba SC 4-0 TRA United | Highlights | CRDB Bank Federation Cup - 17/05/2026

#CRDBBankFederationCup: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya TRA United kwenye mchezo wa robo fainali ya CRDB Bank Federation Cup. Magoli ya Simba yamefungwa na Clatous Chama, Anicet Oura, Selemani Mwalimu na Bashiri Kibaila. Mchezo wa nusu fainali ni Coastal Union dhidi ya Simba SC. FT: Simba SC 4-0 TRA United #KombeLaShirikishoLaCRDBBank #CRDBCup #FACup #SimbaSCVsTRAUnited #SimbaSC #TRAUnited #SimbaTRAUnited



Magoli | Dodoma Jiji 3-2 Yanga SC | NBC Premier League 13/05/2026
Magoli | Dodoma Jiji 3-2 Yanga SC | NBC Premier League 13/05/2026

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC wamepoteza mchezo kwa mara ya kwanza msimu huu, wakichapwa 3-2 na Dodoma Jiji, mchezo, mchezo ukipigwa Airtel Stadium, Singida. Magoli ya Yanga yamefungwa na Allan Okello dakika ya 2 na 41, huku magoli ya Dodoma Jiji yakitoka kwa Bakari Mwamnyeto aliyejifunga dakika ya 29, Mwana Kibuta David dakika ya 90 na Wazir Junior Shemtembo dakika za nyongeza. Haya hapa magoli yote..



TRA United 4-1 Azam FC | Magoli | NBC Premier League - 08/05/2026
TRA United 4-1 Azam FC | Magoli | NBC Premier League - 08/05/2026

#NBCPL: Tazama magoli yote matano yaliyofungwa kwenye mchezo wa NBC Premier League kati TRA United dhidi ya Azam FC. FT: TRA United 4-1 Azam FC Magoli ya TRA United yamefungwa na Ally Ng'azi, Ammy Mapaka na Ramadhan Salum 'Chobwedo' Goli la Azam FC limefungwa na Jephte Kitambala Bola. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #TRAUnitedvsAzamFC #TRAUnited #AzamFC #TRAUnitedAzamFC



Yanga SC 0-0 Simba SC | HIghlights | NBC Premier League 01/03/2026
Yanga SC 0-0 Simba SC | HIghlights | NBC Premier League 01/03/2026

KARIAKOO DERBY | Imepigwa dabi moja ya maana sana kwenye Dimba la Amaan, Zanzibar, Yanga na Simba wakimaliza dakika 90 bila bao, lakini burudani za kutosha. Hii ni mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania



Yanga SC 5-0 JKT Tanzania | Highlights | NBC Premier League 25/02/2026
Yanga SC 5-0 JKT Tanzania | Highlights | NBC Premier League 25/02/2026

Yanga SC imeichakaza JKT Tanzania mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Wafungaji wa magoli haya ni Mohamed Hussein Zimbwe Jr,, Aurellio Depu, Mudathir Yahya, Prince Dube na Shekhan Ibrahim.



Kuwait 4-3 Tanzania | Highlights | Mechi ya Kirafiki 15/11/2025
Kuwait 4-3 Tanzania | Highlights | Mechi ya Kirafiki 15/11/2025

Ni mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA iliyopigwa kwenye Dimba la Al Salaam, Cairo nchini Misri, na timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars kuchwa 4-3 na Kuwait. Magoli ya Tanzania yamefungwa na M’mombwa 6’, 87’, na Taryin Allarakhia 34’ huku ya Kuwait yakitoka kwa Daham 46’, 52’ Nasser 63’ na Hamdan 69’



Maximo asema Brazil, Argentina ni mahasimu ndani ya uwanja
Maximo asema Brazil, Argentina ni mahasimu ndani ya uwanja

KMC vs SINGIDA BS: Kocha Marcio Maximo wa KMC, amesema mataifa ya Argentina na Brazil ni wapinzani ndani ya uwanja, ...