FT: Simba 2-0 Dodoma Jijj ๐ Alama tatu muhimu kwa Simba, Dodoma Jiji wamepoteza mechi ambayo naona walicheza vizuri, walikuwa na nidhamu nzuri ya kuzuia kwa bahati mbaya kosa moja kubwa likawafanya waikabidhi mechi mikononi mwa Simba. ๐ Dodoma Jiji hawakuwaruhusu Simba kupiga penetration passes, walizuia half spaces na kuwafanya wacheze nje ya eneo la hatari muda mwingi, katika system ya low blocks defensive hukuona Simba wanatengenezaje nafasi kabla ya kosa la penati kutokea. ๐ Ipo sehemu ya Simba kujitazama mara mbili, mara nyingi wanapokutana na timu za aina hii wanajenga mashambulizi yao taratibu hiyo inawasaidia wapinzani kujipanga kwa sababu presha inakuwa ni ndogo kwenye eneo lao. ๐ Zipo nyakati ambazo Dodoma Jiji wangekuwa wakatili mbele ya lango la Simba pengine wangeifanya mechi kuwa ngumu zaidi, ni rahisi kukishinda kiungo cha Simba kama utaamua kuwa press na kufanya mikimbio nyuma ya safu hiyo. ๐ Viungo wa Simba wanapitika kirahisi timu isipokuwa na mpira, tofauti ilikuwa ndogo tu, Dodoma Jiji hawakuwa na ubora katika kufanya matendo ya mwisho ya kutengeneza nafasi na kufunga magoli na hii inaficha udhaifu wa wapinzani ulioonekana