Content removal request!


ONA ALICHOKISEMA SHABIKI WA SIMBA ANAEMKUBALI FISTON MAYELE BAADA YA SIMBA KUWAFUNGA DODOMA JIJI

✍Simba SC hawakuwa katika ubora ambao wenyewe wangetamani lakini wamevuna alama 3 , katika mechi zote za msimu ngumu mechi zote ucheze kwa kiwango cha juu , muhimu ni kukusanya alama tatu ndio waliciofanya leo dhidi ya Dodoma FC ambao hawakuonesha madhara kwenda mbele . ✍Dodoma FC dakika kama 5 au 10 za mwanzo walianza na BACK 3 lakini wakaibadilisha haraka na kwenda 4-3-3 wakiwa na mpira na 4-4-2 bila mpira , hawakutaka kuzidiwa idadi ya wachezaji katikati ya uwanja na pembeni ya uwanja... lakini bado mara kadhaa waliacha spaces kubwa sana baina ya mstari mmoja na mwingine na mchezaji kwa mchezaji ✍Ni Simba tu wenyewe , Dodoma ni kama vile hawakuwa na mpango au maono ya kutafuta goli, walikuwa tayari kufungwa ( Dodoma was there for taking ) ...Simba hasa kipindi cha kwanza walikuwa slow sana , umakini unakosekana , walikuwa wanacheza kama wanaongoza 3 au 4 , mpira haukutembea kwa haraka kutoka sehemu moja kwenda nyingine ...viungo watatu ( Chama Nyoni Mzamiru ) + mawinga wawili ( Banda na Sakho ) wote wanacheza mbele ya Dodoma ...hakukuwa na mikimbio ya kutosha nyuma ya kiungo cha Dodoma na safu ya ulinzi ya Dodoma ( Easy to defend ) ✍Nafikiri Dodoma walicheza bila imani kwamba wanaweza kufunga au kupata chochote kitu dhidi ya Simba ,kuna muda walikuwa " Casual " sana , jinsi idadi ya mipira waliyokuwa wanapoteza kirahisi , iwe kwenye kiungo mpaka pembeni ya uwanja ( Sloppy ) nafikiri hata Wawa na Onyango wanaweza wakaangaliana na kujiuliza " Hivi leo mbona hatuna kitu cha kuzuia ? " 😀 NOTE 1: George Wawa sijui alikuwa anafikiria nini ? Alijua refa hatomuona kushika mpira kwa staili ile ? Doh 😀😀 na bado akabisha,Chama Jr alituliza akili licha ya wachezaji wa Dodoma kumfanyia " Mind game" 2: Cleophace Mkandala ..amekosa tu msaada kutoka kwa wenzake,maana ndio mchezaji pekee ambaye akiwa na mpira ndio unaona anaweza kufanya jambo. 3: Positive nyingine kwa Simba ukiacha alama 3 ni kurejea kutoka kwenye majeraha baadhi ya wachezaji 4: Peter Banda hakuacha kujaribu kutengeneza nafasi mpaka akapata assist yake kwa Kagere. Never give up 5: Dodoma inaonekana bado inasukwa ..muda unakimbia FT: Simba 2-0 Dodoma FC