WAPE TABASAMU: Team Kibwana kwa mara ya tatu imekula kichapo safari hii ikipigwa 6-2 na Team Job katika mchezo wa hisani wa #WapeTabasamu2024 uliopigwa Uwanja wa jamhuri. Morogoro. Magoli ya Team Job yametoka kwa Eng. Hersi Said (13'), Said Ndemla (234'), Prince Dube (27'), George Mpole (78'), Samson Mbangula (79') na Edwini , Balua 90'+4. Magoli yote mawili ya Team Kibwa yamefungwa na Saimon Msuva dakika ya 30 kwa free-kick na dakika ya 47 kwa penati. Haya hapa magoli yote manane.
Team Job ambayo iko chini ya beki Dickson Job wa Yanga imeibuka na ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Team Kibwana iliyo chini ya Kibwana Shomary baada ya sare ya 2-2 katika muda wa kawaida, ukiwa ni mchezo wa hisani kusaidia afya ya uzazi ikienda kwa jina la #WapeTabasamu . Yamefungwa magoli manne na wachezjazi wawili katika muda wa kawaida.... Wachezaji hao ni Abdul Suleiman Sopu akiifungia Team Kibwana magoli mawili dakika ya 23 na 50 huku Saimon Msuva akichomoa magoli yote mawili dakika ya 74 na 80. Mechi imepigwa kwenye Dimba la Jamhuri, Morogoro. Shuhudia hapa magoli yote na mikwaju ya penati.