Yamefungwa magoli matatu.... chuma mbili zikiwekwa kambani na Allan Okello na goli lingine likifungwa na Mudathir Yahya kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Hii ni Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
#CRDBBankFederationCup: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya TRA United kwenye mchezo wa robo fainali ya CRDB Bank Federation Cup. Magoli ya Simba yamefungwa na Clatous Chama, Anicet Oura, Selemani Mwalimu na Bashiri Kibaila. Mchezo wa nusu fainali ni Coastal Union dhidi ya Simba SC. FT: Simba SC 4-0 TRA United #KombeLaShirikishoLaCRDBBank #CRDBCup #FACup #SimbaSCVsTRAUnited #SimbaSC #TRAUnited #SimbaTRAUnited
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC wamepoteza mchezo kwa mara ya kwanza msimu huu, wakichapwa 3-2 na Dodoma Jiji, mchezo, mchezo ukipigwa Airtel Stadium, Singida. Magoli ya Yanga yamefungwa na Allan Okello dakika ya 2 na 41, huku magoli ya Dodoma Jiji yakitoka kwa Bakari Mwamnyeto aliyejifunga dakika ya 29, Mwana Kibuta David dakika ya 90 na Wazir Junior Shemtembo dakika za nyongeza. Haya hapa magoli yote..
KARIAKOO DERBY | Imepigwa dabi moja ya maana sana kwenye Dimba la Amaan, Zanzibar, Yanga na Simba wakimaliza dakika 90 bila bao, lakini burudani za kutosha. Hii ni mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania
Yanga SC imeichakaza JKT Tanzania mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Wafungaji wa magoli haya ni Mohamed Hussein Zimbwe Jr,, Aurellio Depu, Mudathir Yahya, Prince Dube na Shekhan Ibrahim.
Ni mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA iliyopigwa kwenye Dimba la Al Salaam, Cairo nchini Misri, na timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars kuchwa 4-3 na Kuwait. Magoli ya Tanzania yamefungwa na M’mombwa 6’, 87’, na Taryin Allarakhia 34’ huku ya Kuwait yakitoka kwa Daham 46’, 52’ Nasser 63’ na Hamdan 69’
KARIAKOO DEEBY | Fahamu ukweli kuhusu matukio yote yaliyozua utata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba uliopigwa Septemba 16, 2025. Moja kati ya matukio yaliyozua gumzo ni goli pekee walilofunga Yanga na kuamua mshindi wa Ngao ya Jamii 2025. Osman Kazi na jopo lake wanamaliza utata kwa kutumia sheria na kanuni za soka
KUTOKA CAIRO MISRI: " ....msimu huu tunahitaji kuwapiku Yanga" Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Wadi Degla FC inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo, Kocha wa Simba, Fadlu davids anaeleza baadhi ya mambo ambayo ameridhika nayo, na maeneo ambayo bado ana kazi ya kufanya.... Kuhusu kikosi chake, Kocha Fadlu anasema bado wanahitaji angalau mchezaji mmoja mwenye kitu cha ziada (X-Factor) atakayewaongezea kitu hasa kwenye michuano ya kimataifa pamoja na mbio za ubingwa wa #NBCPremierLeague msimu ujao wakilenga kuwa juu ya Yanga ... Fadlu anasema anaamini mdhamini wao upande wa jezi, 'Jayruty', atalimaliza hilo.... Naye mfungaji wa moja kati ya magoli mawili ya Simba, Kibu Denis anazungumza machache kuhusu maendeleo ya kambi nchini Misri.... Patrick Nyembera anakuja na taarifa kamli kuhusu mchezo huo... #SimbaSC #SimbaEgypt #SimbaPreSeason