Goli pekee la Clement Mzize limeipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudan katika mchezo wa marudiano, Ligi ya Mabingwa Afrika #CAFCL kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Matokeo haya yameifanya Yanga itinge hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa jumla ya magoli 3-0 kufuatia ushindi wa 2-0 ilioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Kigali nchini Rwanda.