Yanga SC imeichapa Mafunzo FC inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Magoli ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na Balama Mapinduzi dakika ya 19', Heritier Makambo dakika ya 52' na Fiston Mayele kwa penati dakika ya 71' huku Ahmed Maulid na Abdulhakim Naim wakiifungia Mafunzo mabao mawili dakika ya 9 na 55'