Content removal request!


Canavaro: Vijana walipunguza umakini (FT: YANGA 4-3 STAND UNITED)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC leo imepata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stand United katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Mara baada ya mchezo huo, Nahodha wa Stand United Jacob Masawe ameeleza kusikitishwa na matokeo hayo akidai kuwa wao ndiyo waliotengeneza nafasi nyingi kuliko Yanga lakini wakashindwa kuzitumia. Masawe amesema matokeo hayo ni mipango ya Mungu na kwamba watajipanga kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa mjini shinyanga. Kwa upande wa Yanga, Meneja wake Nadir Haroub amesema vijana wake walipoteza umakini baada ya kuona wanaongoza kwa mabao manne, lakini sasa watajipanga vizuri ili kurekebisha makosa yaliyoonekana.