Content removal request!


MTIBWA SUGAR 2-1 COASTAL UNION: FULL HIGHLIGHTS (VPL - 30/10/2019)

Ni mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara , Mtibwa Sugar ikifanikiwa kupata ushindi wa bao mbili kwa moja dhidi ya wagosi wa kaya Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa kwenye dimba Jamhuri mkoani Morogoro. Huu unakuwa ni mchezo wa pili mfululizo Mtibwa wanashinda nyumbani baada ya kuanza vibaya msimu huu lakini kwa sasa wamebadilika na kurejea kwenye kiwango chao kilichozoeleka kutokana na ukongwe wao kwenye ligi. Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Dickson Daud Mbekya na Jafar Kibaya wakati bao la kufutia machozi la Coastala Union likifungwa na Kibailo.