Content removal request!


AL AHLY WAMTAMBULISHA MIQUISSONE/ PITSO AMPA DARAJA LA JUU/ WAANDISHI WA HABARI WASHANGAZWA!

KOCHA Mkuu wa Al Ahly ya Misri raia wa Afrika Kusini, Pitso Mosimane, amemfungukia kwa mara ya kwanza aliyekuwa winga wa Simba, Luis Miquissone kuwa ni mchezaji hatari kutokea Afrika kwasasa na ndiyo maana amemsajili kwenye kikosi chake. Luis aliyejiunga na Simba, Januari 2020, akitokea UD Songo ya kwao Msumbiji, mwishoni mwa msimu huu aliachana rasmi na timu hiyo kisha kujiunga na Al Ahly kwa mkataba wa miaka mitatu. Taarifa kutoka nchini Misri, imeeleza kuwa, tangu Luis ajiunge na klabu hiyo amekuwa gumzo kubwa, jambo ambalo limewafanya waandishi wa nchini humo kumuuliza kocha Mosimane juu ya uwezo wake na kujikuta akimmwagia sifa lukuki. -- Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali tembelea www.dar24.com #simbasc #yangasc #luismiquissone