Content removal request!


Binti kutoka Tanzania ashika nafasi ya pili Afrika mashindano ya kuchezea mpira (Football Freestyle)

Mwanadada Hadhara Mohamed kutoka Tanzania ameshika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Afrika ya kuuchezea mpira (Football Freestyle) yaliofanyika nchini Nigeria. Ushindi huo umemfanya kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya dunia yatakayofanyika nchini Poland November 22 mwaka huu. Mashindano hayo yaliofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika yalishirikisha wanaume na wanawake ambapo kwa upande wa wanawake mwanadada Rasheedat Ajibade raia wa Nigeria ameshinda nafasi ya kwanza mbele ya Mtanzania Hadhara Mohamed. Rais wa chama cha mchezo wa kuchezea mpira Tanzania (TFFA) Morison Moses ameelezea namna walivyopata nafasi ya kushiriki mashindano hayo.