Timu ya Geita Gold FC leo imepata ushindi wake wa kwanza kwenye #NBCPremierLeague kwa kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1, mechi ikipigwa kwenye Dimba la Kaitaba, Bukoba. Magoli yote mawili ya Geita yamefungwa na George Mpole huku Kagera Sugar wakipata bao lao kupitia kwa Mbaraka Yussuph.