KUELEKEA TANZANIA VS BURUNDI: Mkutano na wanahabari ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Hamasa Haji Manara. Baadhi ya wasanii waliozungumza ni Monalisa, Dokii, JB na Steve Nyerere. Pia yupo Katibu Mkuu wa zamani wa TFF Angetile Hoseah. Wapo pia Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred, Kamati ya wanahabari, wasanii wa muziki na filamu pamoja na wadau mbalimbali wa soka. Lengo ni kuujaza Uwanja wa Taifa Jumapili Septemba 8, 2019 ili kuifyeka Burundi.