Timu ya Mbeya City ya Jijini Mbeya imeichapa timu ya Alliance kutoka Jijini Mwanza mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya. Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Victor Hangaya dakika ya 18 na Eliud Ambokile dakika ya 81. Haya ndiyo magoli yenyewe.