Content removal request!


JOTO LA AFRIKA 11/4/2019: Simba inavyoweza kuitoa TP Mazembe Ligi ya Mabingwa Afrika (Uchambuzi)

Kipindi cha #JotoLaAfrika Alhamisi hii kimechambua kwa kina mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe uliopigwa Jijini Dar es Salaam Aprili 6, 2019 na kumalizika kwa suluhu. Pia wachambuzi wetu Ally Kamwe na Charles Abel wametoa mapendekezo ya nini kifanyike ili Simba ipate matokeo mazuri katika mchezo wa marudiano unaopigwa Aprili 13, 2019 na kusonga mbele. Sehemu ya pili ya kipindi tumengalia maandalizi ya timu mbalimbali kuelekea fainali ya mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zinazoanza kutimua vumbi Aprili 14, jijini Dar es Salam.