Content removal request!


SIMBA 4-0 SINGIDA UNITED, VPL HIGHLIGHTS (18/01/2018)

Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC imeinyanyasa Singida United kwa kuipiga mabao 4-0 katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye dimba la Taifa Dar es Salaam. Mabao ya Simba yamefungwa na Shiza Kichuya dakika ya tatu, Asante Kwasi dakika ya 23 na Emmanuel Okwi aliyetokea benchi dakika ya 65 na kufunga mabao mawili dakika ya 76 na 82.