Mabingwa wa ligi kuu ya wanawake Tanzania bara, Simba Queens wameitandika baobab Queens mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo uliochezwa kwenye Dimba la Uhuru, jijini Dar es Salaam. Magoli ya Simba Queens kwenye mchezo huu yamefungwa na Pambani kuzoya dakika ya 2, Asha Jaffary dakika ya 50 na Joelle Bukuru dakika ya 90'