Kikosi cha Simba SC kimeongeza wigo wa pointi kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda FC. Magoli ya Francis Kahata na Deo Kanda kwenye kila kipindi ndiyo yaliyoipa Simba SC ushindi huo huku nahodha wake John Bocco akirejea baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha. Simba SC itakutana na wapinzani wake wa jadi Yanga SC kwenye dimba la Taifa Januari 4 kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.