Content removal request!


Adam Salamba na Baraka Mpenja wafanya bonge la 'Suprise' kwenye Soka Kijiweni

Straika wa Lipuli FC ya Iringa Adam Salamba ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Stand United ya Shinyanga, ghafla amerejea Shinyanga yalikokuwa makazi yake na anakutana na Dodi katika kipindi cha Soka Kijiweni. Amezungumza mengi akiwa na washkaji zake likiwemo lile bao aliloifunga Simba katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli. Katika hali ya kushangaza pia mtangazaji Baraka mpenja kutoka Azam TV ameibuka na kuwapa LIVE lile bao la pili alilofunga Habib Kiyombo wa Mbao FC dhidi ya Yanga, Desemba 31, 2017. Hii ni sehemu ya kipindi kilichoruka Aprili 30 mwaka huu. Kumbuka kipindi hiki kila Jumatatu saa 1:00 usiku, Azam Sports 2.