Lipuli FC leo imeondoka na point tatu baada ya kuichapa Mbao FC katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliopigwa dimba la Samora mjini iringa. Mabao ya Lipuli yamefungwa na Asante Kwasi dakika ya 59 na 73 wakati bao la Mbao likifungwa na Habibu Haji dakika ya 10.