Simba SC wameipa kichapo cha mabao 4-1 Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa Mei 8, 2022 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Waliopachika mabao haya ni Kibu Denis dakika ya 40, Rally Bwalya dakika ya 67, John Bocco dakika ya 82 na Hennock Inonga dakika ya 85 wakati bao pekee la Ruvu shooting likifungwa na Haruna Chanongo, dakika ya 83.