Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF CL) kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mashetani Wekundu wa Nkana FC katika mchezo uliopigwa mjini Kitwe nchini Zambia. Baada ya mchezo huo, Msemaji wa Simba Haji Manara amezungumza na Mshikemshike Viwanjani na kusema kuwa matokeo waliyoyapata siyo mabaya sana, huku akiwataka mashabiki wao kuujaza Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki moja ijao.