Content removal request!


Bao la Donald Ngoma; Kagera Sugar 0-1 Azam FC (TPL - 04/11/2018)

Azam FC imeendelea kujivunia alama tatu za ugenini baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa kaitaba mjini Bukoba. Bao pekee la Azam FC limewekwa nyavuni na mshambuliaji wao Mzimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 40 baada ya kutumia vizuri uzembe wa mabeki wa Kagera Sugar wakiongozwa na Juma Said Nyoso. Hili ndilo bao.