Content removal request!


HIGHLIGHTS: TANZANIA 1-3 UGANDA (CECAFA U17 AFCON QUALIFIER)

Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imetupwa nje ya michuano ya kufuzu AFCON kwa vijana kutoka ukanda wa CECAFA baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Uganda. Mchezo huo wa nusu fainali umepigwa kwenye dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam na kushuhudia Serengeti Boys wakibanwa vilivyo na Uganda ambao walionekana kucheza soka la nguvu zaidi. Uganda walipata bao la kwanza mapema kabisa dakika ya 4 kupitia kwa Abdul Idd kabla ya Serengeti kusawazisha kupitia kwa kona ya moja kwa moja iliyopigwa na Edson Mshirakandi dakika ya 11, na hadi kipindi cha kwanza kinakamilika Serengeti Boys walionakana kuanza kuhimili mashambulizi ya Uganda, na kumiliki mpira. Kipindi cha pili Uganda walikianza kwa kasi zaidi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 76 kupitia kwa John Alou huku bao la tatu likipatikana baada ya beki wa Tanzania Amiri Njilu kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa, dakika ya 90.